Taifa likiingia vitani leo,Itakuwaje?

Dhaifu afunge safari akawaombe wawekezaji waje wapigane! Hivi raia wa Tz apigane kwa ajili ya nini hasa???
 

Umoja na Mshikamano wa Kitaifa kwa sasa hatuna kabisa na hii inatokana na Udhaifu wa Uongozi wa Juu hasa Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi. Tanzania inahitaji kiongozi mwenye uchungu na Nchi yetu ambapo kwa sasa hatuna viongozi wa namna hii. Tulionao wote ni viongozi wachumia tumbo tu. Natamani kama ningezaliwa Kenya au Rwanda.

Wanachoweza ni kupambana na haki za Wananchi bila sababu huku wakiunda sheria kandamizi bila sababu. Tukianzisha vita saa hizi lazima tuchapwe kichapo kitakatifu sana. Maana Nchi imejaa udini, ufisadi, watu kujichumia mali ya Nchi kama zao. Mungu utubariki tusipigwe mmpaka umoja na mshikamano utakapo fufuka tena.
 
Ahhh!! Hapa Kichapo kwa kwenda Mbele kwani mafisadi wameshajenga New Jesey

Huo ndio wakati mzuri wa kumjua mzalendo wa kweli, mafisadi watakimbia na sisi ambao tunaojipambanua kuwa ni wazalendo tutafanyaje?
 
Hilo halitakuwa jambo la kutuumiza kichwa sisi watanzania bali itakuwa vita ya nchi zote zenye uwekezaji wa kifisadi hapa Tanzania kupitia Makampuni yao ili kutetea maslahi yao. Tena nahisi Marekani kaenda Malawi kuchagiza hilo maana tunajifanya tumemsahau na kumkaribisha mchina kwa kishindo
 
Haaaapa tuombe tu vita istokee kwani tutachapwa hadi tutawaliwe na na kukaliwa juu na Malawi (Joyce Banda). Mwaka 1978 tuligangamala vijana wa mujibu wa sheria JKT, leo sijui mtampeleka nane frontline labda Nape na Ridhiwani
 
......ni mke na mume wapumbavu tu ndio watakao endelea na malumbano kuhusu uaminifu ktk ndoa yao huku wakimuona jambazi akivunja mlango na wasifanye kitu........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…