Taifa langu linaangamia....

Taifa langu linaangamia....

Masanilo

Platinum Member
Joined
Oct 2, 2007
Posts
22,282
Reaction score
4,556
Kitendo cha mtuhumiwa wa madawa ya kulevya kuendelea kuwa huru, Kama vile taifa hili halina vyombo vya ulinzi na usalama, najiuliza maswali mengi bila majibu. Pamoja na udhaifu wa raisi Kikwete kwa hili huyu bwana Azan ili bidi Mara moja awe rumande na uchunguzi Mara moja uanze. Kama hili hawezi basi anipe mamlaka Mimi Mara moja nitathibitisha huyu Mbunge Mali zote anazomiliki ni zao la biashara hii haramu. Kukamata mtandao wake ni rahisi Kabisa kuliko ilivyokuwa kumtesa Dr Ulimboka. Ndani ya serikali hii kuna mtandao wenye nguvu kuliko dola wakiendesha biashara hii bila woga, hata huyu Mbunge naye ni kibaraka Mkuu wao yuko na anajulikana. Hakamatiki maana serikali itayumba. IGP Mwema na Othman Rashidi hebu fanyieni Zuri nchi yenu. hakuna sababu za kisiasa huyu bwana Idd Azzan ni drug dealer wa Muda mrefu.
 
Likisemwa jambo sana ni lazima kulifanyia kazi bila kuupuza,,nadhani ingekuwa sahihi dola kumweka rumande huyu Mbugu Azan,,hii itampa usalama kwa jamii inayomzunguka pia kurahisisha kupata ukweli wa kauli ya muuza madawa haya aliyekamatwa huko China.
 
Serikali ya kishikaji ukiongezea na udhaifu ndiyo balaa zaidi
 
Masanilo tatizo tunalozidi kulilea ni kwamba tunachodhani ndiyo dola yetu, nacho kinaongozwa na dola yake! Na hiyo dola yake siyo ya kuwalinda wananchi bali ni kikundi cha watu walioteka madaraka, kubaka uchumi na kuhodhi mali ya umma.
 
Kitendo cha mtuhumiwa wa madawa ya kulevya kuendelea kuwa huru, Kama vile taifa hili halina vyombo vya ulinzi na usalama, najiuliza maswali mengi bila majibu. Pamoja na udhaifu wa raisi Kikwete kwa hili huyu bwana Azan ili bidi Mara moja awe rumande na uchunguzi Mara moja uanze. Kama hili hawezi basi anipe mamlaka Mimi Mara moja nitathibitisha huyu Mbunge Mali zote anazomiliki ni zao la biashara hii haramu. Kukamata mtandao wake ni rahisi Kabisa kuliko ilivyokuwa kumtesa Dr Ulimboka. Ndani ya serikali hii kuna mtandao wenye nguvu kuliko dola wakiendesha biashara hii bila woga, hata huyu Mbunge naye ni kibaraka Mkuu wao yuko na anajulikana. Hakamatiki maana serikali itayumba. IGP Mwema na Othman Rashidi hebu fanyieni Zuri nchi yenu. hakuna sababu za kisiasa huyu bwana Idd Azzan ni drug dealer wa Muda mrefu.

Suala la madawa ya kulevya sio la Jk mbona sisikii wapinzani wakiliongelea? kila mtu kawa bubu hata JK anapima upepo pia kama binadamu wengine
 
...mbona sisikii wapinzani wakiliongelea? kila mtu kawa bubu hata JK anapima upepo pia kama binadamu wengine
Tembelea CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya.
TAMKO LA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. VINCENT JOSEPHAT NYERERE (MB) KUHUSU UDHAIFU WA SERIKALI KATIKA KUKOMESHA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI........................................................................................................................................
........................................................................................................................................

MUHIMU: IKIWA SERIKALI ITAENDELEA KUPUUZIA JAMBO HILI AMBALO LINALIANGAMIZA TAIFA, BASI KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI ITAENDESHA OPERESHENI NCHI NZIMA ILI WANANCHI WAPIGE KURA KWA WAHUSIKA WAKUU WA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, NA BAADA YA ZOEZI HILO, TUTAANIKA HADHARANI (KWA KUWATAJA MAJINA) WAHUSIKA WA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA.

Vincent Josephat Nyerere (Mb)
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA WAZIRI KIVULI WA MABO YA NDANI YA NCHI
Imetolewa leo, tarehe 16 Julai, 2013
 
Maana yangu ni kwamba silisikii likiimbwa majukwaani kama ufisadi au nawao wamo
Lini umesikia wanasiasa (Upinzani na Utawala) wakishikia bango suala la Afya au Elimu majukwaani ukiachilia ushabeki wa msimu pale yanakuwa yameishatokea majanga? Siasa zetu ni za kuwaza uchaguzi na "nitoke vipi" siyo za kujadili issues, kutafuta suluhisho na kuleta maendeleo!
 
Suala la madawa ya kulevya sio la Jk mbona sisikii wapinzani wakiliongelea? kila mtu kawa bubu hata JK anapima upepo pia kama binadamu wengine

Mkuu JK ni kinara ndiyo maana Hana meno Kabisa na madawa haya
 
Mtuhumiwa angekua Mh Msigwa au Lema
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Hahaha saizi wangekuwa hawatamaniki! ila kwasababu wote ni watu wahayo madili hakuna wakumgusa mwenzie wakiguswa nchi itayumba, ila hawa watu mimi nafikiri uma sasa inabidi iwatathimini vinginevyo kila siku tutakuwa tunapiga kelele hapa bila ufumbuzi, wanachotaka nikukifanya hiki kizazi kiwe cha mataahira ili watoto wao na wajukuu wao waje kutawala bila stress.
 
Ndio maana naona afadhari ya utawala wa kina chief mangungo na carl paters coz yanayofanyika sasa kwa TZ ni zaidi ya sodoma na gomola, kifo cha magamba kimewadia.na wataendelea kuumbuana sana zaidi ya tuonavyo sasa.
 
Back
Top Bottom