Taifa katika hatihati ya kurudi gizani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa katika hatihati ya kurudi gizani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Apollos, May 6, 2012.

 1. A

  Apollos New Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itv wameripoti hali mbaya ya kina cha maji mtera wakati na mvua ndo izo zinakatika bwawa halijajaa. Maskini wabongo tutaendelea kuhofia umeme wa maji mpaka lini.
   
 2. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutaendelea kucharazwa na bakora ya mgao wa umeme mpaka Serikali itakaposhika adabu, na kutenganisha Siasa na masuala ya Uchumi! Ukuaji wa Uchumi unaambatana na uwekezaji katika sekta ya Nishati na miundo mbinu, na wala si vinginevyo! Tunawekeza kifisadi, kwa masilahi ya wlio na uwezo na walio madarakani! Tuko tayari kukodi mitambo kwa gharama za mabilioni kuliko kuzitumia kujengea mitambo mipya! Kwa ufupi Serikali haitaki kulimaliza tatizo la Umeme. Ni kitega uchumi Mujaarab kwa waheshimiwa!
   
 3. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msihofu, prof. muhungo has the solutions.
   
 4. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lini tutafika!!!!
   
 5. fige

  fige JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vema na inapendeza biashara yeyote ndani ya Nchi ikafanywa na wazalendo.
  Tatizo letu watz tunapenda kuvuna tusipopanda.Ndio maana tukiwekeza kiujanjaujanja tu.Utakuta kampuni inaitwa ya mtu fulani na haina wana hisa wala mtaji (kimaandishi ina hisa na mtaji na uwezo na ni ya watu wengi).
  Lingine,ni ile tabia ya watz kuwacheka viongozi wazalendo wasiojilimbikizia mali pindi wanapoachia madaraka na kuishi maisha ya kawaida.
  Utakuta watz wanamshangaa aliyekuwa waziri kwa kutokuwa na usafiri wa uhakika.Hali hii hufanya viongozi wengi kutumia vibaya madaraka yao ili wasijechekwa badaye.


  KWA PAMOJA TUJIREKEBISHE KWA KUBADILISHA MITAZAMO YETU.
   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...hohohohooooooooo!!
  Labda..
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hari inazidi kuwa mbaya kwa shirika la umeme Tanzania TANESCO hasa katika swala la miundo mbinu chakavu na linahitaji sh. Tril 1.2 ili lifanye ukarabati wa miundombinu yake la sivyo gizani kama kawa.

  Na mkurugenzi wa Tanesco kadai ukarabati huo unaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.

  My Take

  Si safari za Jk mbili hadi tatu si ni sawa na gharama hizi za kukarabati miundombinu ya Tanesco?
  Kupanga ni kuchagua kama tunachagua safari badala ya maendeleo sijui

   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  TANESCO nayo sasa inaanza kuwa janga la Kitaifa. Kila kukicha haina hela za uendeshaji na kila kukicha inapandisha bei za umeme. Hii ni nini sasa? Mwaka juzi wamepata syndicated loan nasikia tena wako kwenye negotiation ya loan nyingine bado wanahitaji Trillion 1.2!

  Nadhani TANESCO inahitaji restructuring ya hali ya juu sana. Kwanza ifanyiwe due diligence na wataalam wa fedha ili kuangalia wanadai/daiwa kiasi gani, mitambo yao ikoje na hizo njia za kusafirisha umeme zikoje na zinahitaji nini. Kisha igawanywe kuwe na kampuni ya kuzalisha na ya kusambaza umeme.

  Haiwezi ikawa kila siku ni kilio cha pesa na vitisho vya kuingizwa gizani. Sipendi ile hali ya kuingia gizani ijirudie.
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi mmeshasahau kuwa mwaka huu wa budget 2011/2012 walipewa kiasi hicho cha fedha (trillion 1.2) na wakaahidi mgao wa umeme utakuwa historia!
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  MW 5000! Hahaaaaaaaaa!
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Inaongozwa na watu wasio na weledi wa namna ya kuendesha shirika kama lile...bahati mbaya inaanzia juu kabisa, bodi yao na hatimaye kwenye uongozi wa Tanesco.
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hali hii ya Tanesco imesababishwa na Mkapa kupitia sera ya uza uza na menejimenti za kukodi Net Group Confusion. TTCL imenusurika kidogo tu, kama hatutakaza misuli nayo itakwenda harijojo.
   
 13. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kimbunga, mbona hata sasa Tanesco imeshaanza kuwa kampuni ya kusambaza umeme? Songas, Symbion/Dowans wanazalisha na Tanesco wanasambaza na miaka michache ijayo Artumas na Brazil (Stigler gorge) watazalisha na Tanesco watafanya uwakala.
  Siamini kama Tanesco ikigawanywa na kuwa kampuni ya kusambaza itasaidia vinginevyo serikali (mdaiwa mkubwa na sugu) wawe walipaji na Zanzibar walipe bei halisi.
   
 14. y

  ybest Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama vip JK haaghailishe hiyo safari yake aliyoalikwa Marekani na Obama kwa ajili ya hiyo G8 meeting, badala yake hawape hao "good 4 nothing" tanesco!!!!
   
 15. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  UUUUUUUUUUUUUUUUUwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii twaaaaaaaaaaaaaaafwa. Jamani PPF tuliwakopesha BILIONI 15, zitalipwa kweli hizi pesa za wanachama maskini? PPF tuanze mchakato wa kufutilia mbali hii hasara.
   
 16. T

  Tewe JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Tatizo hapa serikali haiwezeshi tanesco kuwa na mipango ya muda mrefu, mara kwa mara serikali imekuwa ikiwekeza kwa mipango ya dharula na kusherehekea ushindi kumbe miundombinu inazidi kuoza, mabwawa yanajaa tope, vyanzo vya maji vinaharibika na kukaushwa haya yote ni mambo yanayohitaji uwekezaji wa muda mrefu na kuacha blaa blaa.

  Kikubwa zaidi ni kwamba niaibu kwa hali yasasa kutegemea maji ya mabwa yanayojaa tope wakati tuna falls za asili, tuna gas ya kutosha mahitaji ya ndani na kuuza nje pia, tuna upepo wa mwingi singida na makambako, kuna uwezekano wa kuzalisha umeme kwa kutumia joto ardhi wakala wa umeme vijijini REA ana raslimali jua isiyoisha, tuna bio energy mashamba ya katani yanaweza zalisha umeme kwa matumizi yao na biashara, mashamba ya mifugo yaweza toa bio energy, vyoo vyaweza toa umeme.

  Kwanini maji? Kwanini mtera? Kwanini kihansi, kwanini nyumba ya mungu? Kwanini lakini?

  We are not serious nahii yote ni kwa ajili ya kulea wachumia tumbo na sera zao zilizoshindwa, let us awake and fight for true freedom & development of our nation.
   
 17. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  Source Mwanahalisi

  Taarifa na barua aliyo andikiwa rais Jk na mwenyekiti wa bodi wa Tanesco Jen. P. Mboma kuwa hali na mstakabali wa shirika hilo kuwa na uhakika wa kuzalisha umeme kulingana na mahitaji yako mashakani na mgao wa umeme hautaepukikwa kama hali ya mambi hayatarekebishwa mapema.

  Miundombinu ileile wakati mahitaji yanaongezeka kila siku. " tunafanya mambo yale yale tukitarajia majibu tofauti"
   
 18. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,518
  Trophy Points: 280
  Taarifa ndani ya serikali zinasema.

  1. Tanesco inaelekilea kufikisika

  2. Mabwawa ya kuzalishia umeme karibu yaishiwe maji

  3. Hakuna fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha maji

  4. Makamouni ya mafuta yanameza karibu kiasi chore kinachokusanywa.

  5. Presha au mkandamizo unaotoka Songosongo ni ndogo mno.

  Tayari mgao wa uneme umeanza katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Mwanza, Mbeya na Shinyanga.
   
 19. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  ....Armageddon
   
 20. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....Armageddon

  Ama ni gharika ya Nuhu Tena
   
Loading...