mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Na Ezekiel Kamwaga
JANUARI 26 mwaka huu, Bunge la 11 linakutana kwa ajili ya Mkutano wake wa Pili. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Bunge hili kukaa na kujadili mambo ya kitaifa kwa vile katika Mkutano wa Kwanza, kazi kubwa ilikuwa ni kuwaapisha wabunge na pia kuzinduliwa kwake.
Hili ni Bunge la aina yake katika historia ya nchi yetu. Hili ni Bunge litakalokuwa na idadi kubwa ya wabunge kutoka Kambi ya Upinzani kuliko lingine lolote katika historia yetu.
Ni matumaini yetu kuwa hili litakuwa ni Bunge lenye kujadili hoja kwa umakini wake, uzito wake na umuhimu wake kwa nchi yetu. Hatutaraji kuona Bunge litakalotawaliwa na itikadi za kivyama.
Wabunge waliochaguliwa kwenye Bunge hili wanatakiwa kufahamu kuwa wanapoingia ndani ya ukumbi wa Bunge, wanatakiwa kuviacha vyama vyao vilivyowaingiza bungeni mlangoni.
Maslahi ya Taifa yanatakiwa kuwaongoza kwenye mijadala yao. Inapofika wakati wa kuchagua baina ya maslahi yao binafsi, ya vyama vyao au nchi yetu, wao wanatakiwa kuweka mbele utaifa. Hatutarajii kuona wabunge wetu wakichapana Makonde ndani ya ukumbi ule maarufu wa Dodoma. Hatutarajii kuona wabunge wakitumia lugha za kuudhi na matusi mbele ya wenzao.
Watanzania wengi wanapata elimu ya uraia kupitia Bunge. Wanaposikiliza mazungumzo ya wabunge wao, wanapata kitu cha kujadili pale walipo. Ni vema wabunge wakawapa wananchi wao mambo mema ya kujadili.
Katika nchi yenye watu masikini kama Tanzania na yenye changamoto lukuki, ni dhambi kwamba wananchi wanapata muda wa kujadili mambo ya hovyo na yasiyo ya msingi yanayofanywa bungeni.
Wananchi wamewapa wabunge wao fursa ya kuisimamia serikali. Fursa ya kutunga sheria zenye maslahi kwa walio wengi. Fursa ya kuhakikisha serikali inatimiza wajibu wake kwa raia wao. Wakifanya nje ya hapo, watakuwa hawajawatendea haki watu wao waliowaamini.
Ni kwa sababu hii, tunataraji kuona Bunge ambalo limeweka mbele maridhiano badala ya mifarakano.
Kwa kusema hivyo, hatumaanishi kuwa tunataka Bunge lililopoa na linaloboa. Tunataka kuona uzalendo, akili, mapambano na mbinu zinazokubalika za kisiasa. Vyombo vya habari vinahitaji haya.
Kazi kwenu wabunge.
CHANZO: Raia Mwema