Tahadhari: Uporaji mkubwa kesho uwanja wa taifa

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,217
Habari wana jamvi? leo nimekuja kuwakumbusha tena kesho ni siku nzuri kwa wapenzi wa club ya yanga na kwa taifa kwa ujumla,kesho ni mpambano kati wababe wa kongo na Tanzania yaani Tp mazembe vs Young African.

Naomba niwakumbushe wadau wote watakao hudhuria mchezo huo kesho,kesho tuna tumaini uwanja utafurika sana,na ikumbukwe kiingilio hakuna kwa hiyo kesho kutakua na vikundi vya uporaji barabarani hasa wakati wa kutoka jioni.

jamani tuwe waangalifu hawa vijana huwa wanapita wanakimbia barabarani wakikukuta na simu mkononi yao,na ukumbuke wanatembea wengi tena wakiwa na mapanga,visu na bisibisi.Unapotoka hakikisha unatembea kwa tahadhari,ikiwezekana simu yako wacha home.

kesho kutakua na wakabaji kutoka

magomeni
manzese
kigogo
keko kwa ujumla
mbagara
yombo

Na mtakao kuwa kwenye magari hakikisha MNAFUNGA VIOOO.Kesho ni siku ya jeshi la polisi kuonyesha uwezo wao wa kiutendaji.

zubedayo_mchuzi.
 
Je una hamu ya kuibiwa, kusukumwa, kukanyagwa, kupigwa virungu, kupoteza wallet, pesa na documents zote, kupigwa mabomu ya machozi, kuibiwa simu na kadhia za kila namna? Basi njoo uwanja wa Taifa leo
 
Je una hamu ya kuibiwa, kusukumwa, kukanyagwa, kupigwa virungu, kupoteza wallet, pesa na documents zote, kupigwa mabomu ya machozi, kuibiwa simu na kadhia za kila namna? Basi njoo uwanja wa Taifa leo
wacha kuwatisha wenzio
 
Hahahahaaaa....... ni hatari aisee. Umefanya vizuri kutekeleza amri ya kuwataarifu walioko njiani au majumbani wabaki huko huko. Uwanja umejaa na walioko nje ni wengi sana. Mabomu yalikuwa muhimu. Mara nyingine wasikurupuke kuweka mechi bure. Kiingilio kingekuwa hata elfu 2 watu wasingekuwa wengi hivi maana kuna vijana wengi sana toka buguruni na viunga vilivyo ndani kilomita 10 wametembea kwenda uwanjani. Ina maana hata nauli hawana. Mechi ingekuwa na kiingilio japo kidogo ina maana hawa wangekaa nyumbani. Maamuzi ya aina hii kwa jiji kama hili ni kuwatakia vijana majeraha na vifo. Nawapa pole waliojeruhiwa.
 
Back
Top Bottom