Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,222
- 157,418
Wadau kuna wizi mpya unatumika naomba niwaeleze. Tukio limetokea Tegeta, Dar leo 26 Machi 2017 saa 8:00 mchana huu.
Nilipaki gari pembeni mwa barabara Tegeta kwa Ndevu upande wa kanisa, ndani ya gari nilimuacha mama, shemeji yangu, na watoto wawili.
Nilitoka kwenda kununua begi la mtoto na wife alienda kumnunulia mtoto wetu vifaa vya shule maana tulikua tunaenda kumtembelea shuleni.
Sasa wakati nimewaacha wale ndugu kwenye gari, kuna mtu alikuja akawauliza dereva wa gari yupo wapi? Wakamjibu kwamba alitoka, akawaambia gari yake ipo nyuma imeharibika alihitaji msaada, wakamwambia sipo basi akaondoka.
Nilivyorudi nikaambiwa nikawa nasubiri kwenye hiyo gari iliyokua nyuma yangu aliyosema ni ya kwake lakini gari ilikua locked na ndani hakukua na mtu. Niliamua kukaa kwenye gari na ndugu waliobaki humo tunamsubiri wife, mbele yangu kuna gari Vitz ya dark blue ilikua imepaki namba T520 DDA, aliyepaki sikumuona maana tulikuta imepaki hapo.
Ghafla nikaona jamaa mmoja hivi mtanashati kavaa shati ya mikono mirefu, kasimama pembeni mwa hiyo gari, alikua na mfuko wa Rambo "plastic" mweusi kauweka juu ya hiyo gari. Ghafla alitoka nakuacha mfuko juu ya gari kasogea mbele ya kanisa kwenye miamvuli wanapouza machinga,akawa anavuta sigara.
Ghafla nikaona dada mmoja kaja kwenye hiyo gari akawa ameshika funguo, akataka kufungua ghafla akaona mfuko mweusi juu ya gari yake. Hakufungua akaja kwangu nakuniuliza kama nilimuona aliyeweka mfuko juu ya gari yake. Nikamwambia niliomuona , naweza kumtambua nikimuona, basi nikatoka kwenye gari nikaangaza macho, ghafla nikamuona yule mwanaume anavuta sigara karibu na miamvuli kwa machinga.
Kwa ujasiri nikamwambia yule dada kwamba aliyeweka mfuko pale juu ya gari ni yule huku nikimuonyesha kwa kidole. Tukamwita nakumuuliza kwa nini aliweka mfuko pale juu? Alijibu alifikiri ni taxi, nilivyokua na hasira, maana niliwahi ibiwa, nilishangaa namsogelea nimchape, aligundua hilo baadae akabadilisha maada.
Akasema samahani hii gari niliifananisha na gari yao wamepaki nyuma, nikasema nipeleke mlikopaki, akatuonyesha gari ya silver ambayo sio Vitz pia, nikamuuliza hii gari na ile vifananaje? Akasema samahani ni ile nyuma, akatuonyesha nyingine nikasema twende, tukakuta ni tofauti kabisa.
Nikamuomba yule dada aniruhusu nimshughulikie mwizi, naona dada alijawa na Ukristo sijui Uislam, akasema tumuache.
Hili sio tukio la kwanza kunitokea Tegeta kwa Ndevu ndani ya mwezi huu, wiki mbili zilizopita nikiwa nimepaki gari hapo hapo alitokea jamaa mmoja kama anatujua, anajua tunaishi wapi, akasema samahani najua nyinyi mnakaa sehemu fulani karibu na wapemba fulani, akitaja sehemu tunayoishi, kweli kuna mpemba ni jirani yetu.
Akasema mimi nina gari imeishiwa mafuta naomba mnisaidie pesa ya mafuta, akasema anaenda kuchukua watoto wake wanasoma Feza School. Mimi nikamuuliza wife , huyu jamaa watoto wanasoma Feza lakini anaishiwa mafuta? Feza ni shule mojawapo ghali sana hapa nchini. Baadae tukamwambia hatuna kitu akasema Mungu awabariki, akasema ana ndugu zake waPemba pale Tegeta ila wote wameenda kulipa kodi TRA mjini.
Nikajiuliza iweje waPemba wote waenda kulipa kodi kwa pamoja? Kwanini waende mjini wakati TRA wapo Tegeta Kibo Complex? Kwanini wasimtumie pesa kwa mtandao wa simu? Nilijiuliza sana ila sikupata majibu.
Hii ya yule mama leo, nafikiri yule mama angeondoka wangemkimbilia kwamba kawaibia mzigo, kwa sababu jamaa aliyeweka mzigo alijibana karibu na hiyo gari, si walijua kilichokuwemo kwenye mfuko? Nina imani kabisa walimuona wakati akipaki gari na waliona yupo pekee yake.
Ombi langu kwenu, ukipaki gari sehemu kama kuna magari mengine yaangalie na uwaombe wakuangalizie, pia unaporudi kwenye gari hakikisha unaikagua kwa kuizunguka kabla ya kuwasha na kuondoka.