Tahadhari: Serikali ijitazame | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari: Serikali ijitazame

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurtu, Jun 6, 2011.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali inavyo vyombo vya kutosha kuweza kupata taarifa za vihatarishi vya amani na usalama wa nchi. Kwa kutumia taarifa hizo ndipo jukumu la kujilinda au kuzuia usalama wa nchi usipotee hutekelezwa.

  Kwa ugumu wa viongozi ambao hutakiwa kuchukua hatua wanaacha kufanya majukumu yao ya kuchukua hatua na hatimaye nchi nyingi inaingia katika matatizo yasiyo ya lazima kutokea. Wananchi wanapotoa madai yao ya msingi dhidi ya serikali hayazingatiwi wala hayatiliwi maanani. Wananchi wanapochoka kurudia madai hayo watayadai kwa nguvu za ziada na hatimaye kuiondoa serikali madarakani.

  Tumeona wenzetu katika nchi za Kiafrika kama Tunisia, Misri na Libya na nchi zingine za Kiarabu yaliyowapata. Kwanini inatokea hatua ya wananchi kuingia barabarani na kumwondoa kiongozi wao? Kupata sababu hatuhitaji kwenda kufanya utafiti bali zinafahamika kwa viongozi lakini kumbe wanazembea kuchukua hatua.

  Ni wazi kuwa Tanzania tumeanza safari ya kuelekea huku walikofika wenzetu hao wa Tunisia, Misri na Libya. Wananchi wa Tanzania wasidhaniwe kuwa ni watu wa amani kwa maana ya viongozi wetu wanavyotaka tuamini. Kamwe Watanzani wasidhaniwe kuwa wataacha kuiondoa serikali madarakani kwa kigezo cha kuwa nchi hii ni kisima cha amani. Tukiwadhania Watanzania kuwa wako hivyo basi tutakuwa tunapotosha ukweli na kujidanganya wenyewe.

  Dalili zilizoanza kujitokeza zisipuuzwe kamwe na wala Watanzani wasidhaniwe kuwa hawana uwezo wa kuichukulia hatua serikali kama walivyofanya wananchi katika nchi zingine. Mdharau mwiba mguu huota tende.
   
 2. M

  Mboja Senior Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kitendawili. Mdharau mwiba? NI KIKWETE.:A S 100:
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna kila dalili ya kuanguka kwa utawala tulionao. Na swali sio kwa vipi ila casulities watakuwa wanani/wangapi. Kama wewe ni mfuatiaji mzuri wa ccm utagundua kuwa factor kubwa ya kuanguka kwa watawala inaanza na migogoro ya ndani. CCM sasa hivi ni vipande vipande tena beyond reppair! Hii tabia ya kusema Tanzania ni 'tofauti' niseme ndio kama jembe la kichimba kaburi. Watanzania ni kama watu wowote duniani na hata hali ilivyo sasa hivi inadhihira hilo.

  Wako watu wawili wanaweza ku-delay mageuzi (nasema delay na siyo kuzima) nao ni Kikwete na Speaker Anna Makinda. Lakini nina wasiwasi wataendelea na kichwa ngumu bila kujuwa kwa kufanya hivyo wanazidisha kasi ya mageuzi. Kwa maneno mengine ccm ndio watajimaliza wenyewe. CHADEMA on the other hand wanatakiwa kujiandaa kuanzia sasa kuchukuwa majukumu. It is coming.
   
 4. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwaani makinda ni speaker? au ni kivuli cha speaker? yule kijeba? kama ni huyo hana uwezo wowote wa kuchelewesha jambo lolote ambalo CDM kwa kuungwa mkono na wananchi watakalo kuwa wameamua. huyo JMK ajiandaye kujibu udhalimu wake anaoendelea kuufanya kwa kuhamasisha mauaji ya raia wake kwa makusudi kwa kutumia vyombo vyake vya dola. The clock is ticking.
   
 5. k

  kakin Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani kikwete si m.a.v.i
   
 6. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Duuuh! Ina maana unaongozwa na m.a.v.i? Pole sana!!
   
 7. M

  Moses msisia Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hao viongozi wa ccm sio wapenda maendeleo.wamemtoa samwel sitta who was the right person halafu wakamuweka huyo mjinga ili alinde mafisadi hakuna mtu hapo ubabaishaji mtupu .sijui mungu tumemkosea nini watanzania may god save this country
   
Loading...