Tahadhari picha inatisha: Mwanamke auawa na kuwekwa ndani ya jaba la maji

msangi360

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
283
308
Taarifa ya tukio kwa kirefu
Kosa: Mauaji
picha.jpg

Mnamo tarehe 07/03/2017 saa 17.00hrs mtoa taarifa (ke), chaga, 30yrs, kibamba 24yrs, anaeleza kuwa majira ya saa 10.00hrs huko Kibamba alitumiwa meseji kwenye simu yake iliyosema '' nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani'' kupitia namba ya simu ya dada yake ambaye ni marehemu (ke), digo, 34yrs , mama wa nyumbani, mkazi wa Kibamba.

Baada ya kupata ujumbe huo aliogopa na kuanza kuwatafuta ndugu zake wengine na ndipo majira hayo aliamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ambapo baada ya taarifa kupokelewa, aliongozana na askari mpaka nyumbani kwa marehemu na kukuta, gari yake No T 827 CYS aina ya Nissan Moco ikiwa nje ya uzio wa nyumba yao ambapo inasemekana ilikuwepo eneo hilo tokea tarehe 2/03/2017, baada ya kuingia na kuvunja mlango wa chumba cha kulala ulikutwa mwili wa marehemu ukiwa umeharibika na kuwekwa ndani ya jaba la maji.

Uchunguzi wa awali;
Eneo la tukio unaonyesha kuwa marehemu ameuawa aidha na mume wake aitwaye (me) Nyamwezi, umri haufahamiki, JWTZ kambi yake bado kufahamika ambaye kwa sasa inasemekana yuko Zanzibar kwa mafunzo na kuna mashaka makubwa ya kuhusika na mauaji hayo kwani eneo la tukio vimekutwa vipimo vya HIV vikiwa vimetumika ambavyo alipenda kuvitumia kwa kupima afya yake na inaaminika kuwa huenda baada ya kubaini kuwa kuna tatizo hilo ndipo alifanya maamuzi hayo.

Aidha hata kwenye simu yake hapatikani. Uchunguzi unafanywa kujua alipo mume wa marehemu ili aweze kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo. Mwili umehifadhiwa hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi.
Tukio limekaguliwa na OC CID Kimara ASP Boniface, Insp Glory na kundi la makachero.

Taarifa kamili inafuata

=====

Aliyemchinja mke wa mwanajeshi Dar asakwa

JESHI la Polisi limeanza uchunguzi mkali kuwatafuta waliohusika kufanikisha mauaji ya kinyama ya Samira Masoud (34), ambaye ni mke wa mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,  SACP Susan Kaganda.jpg

KAMANDA WA MKOA WA KIPOLISI KINONDONI, SACP SUSAN KAGANDA.

Samira aliuawa nyumbani kwake, eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam, na kisha mwili wa marehemu kukutwa ukiwa kwenye chombo kikubwa cha kuwekea maji cha namna ya beseni.

Akizungumza na Nipashe jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, SACP Susan Kaganda, alisema mwili wa Samira ulikutwa
Jumanne ya wiki hii baada ya taarifa kupatikana kutoka kwa ndugu wa marehemu, ambaye ni mke wa mwanajeshi wa JWTZ (jina linahifadhiwa).

Akisimulia zaidi, Kamanda Kaganda alisema kuwa Jumanne ya wiki hii, majira ya saa 11:00 jioni, ndugu wa marehemu walifika katika kituo cha polisi kutoa taarifa kuhusu marehemu ambaye ni dada yao.

Alisema ndugu hao waliwaeleza polisi kuwa, kwa muda mrefu walikuwa hawana mawasiliano na dada yao, lakini siku hiyo (Jumanne), walipokea ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi ya Samira.

Kamanda alisema ujumbe huo ulikuwa ukisomeka kuwa, “Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu… itaozea ndani.”

Alisema baada ya kuona ujumbe huo, ndugu hao walikwenda nyumbani kwa marehemu, lakini hawakuingia ndani baada ya kukuta gari lake lipo nje ya uzio. Waliamua kwenda kutoa taarifa polisi.

Aidha, alisema baada ya taarifa hiyo, polisi kwa kushirikiana na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kibamba, walifika eneo hilo na kuvunja nyumba na ndipo walipokuta mwili wa marehemu kwenye chombo cha maji huku ukiwa umeharibika vibaya.

“Tumejaribu kila mara kuipiga simu ya marehemu ambayo ilitumika kutuma ujumbe kwa ndugu wa marehemu, lakini imezimwa…mume wake ambaye ni mwanajeshi wa JWTZ, ambaye alikuwa kwenye mafunzo ya kijeshi visiwani Zanzibar, alikuja baada ya kupewa taarifa za kifo cha mke wake. Hivi sasa bado hakuna anayeshikiliwa,” alisema Kamanda Kaganda.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwamba, hivi sasa wanasubiri ripoti ya daktari ili kujua kwa kina namna Samira alivyouawa.
 
Lakini kwanini wasiwahusishe tcra ili wajue sms ilitumwa kutokea mnara wa eneo gani, haiwi sahihi kwa 100% lakini inatoa clue ya kujua aliyeitumia simu mara ya mwisho alikua wapi.

Halafu kuna hilo swala la mume kutojulikana na ndugu wa mkewe, kwamba walikua hawajaoana? Kama hadi wamejua kua hua anapenda kujipima kwa hivyo vipimo means wanamjua.
Na mtu yuko Znz so uchunguzi ndiyo umesimama mpaka arudi? Akirudi akitoa alibi yenye nguvu mtakua mmepoteza muda gani hapa kati?
 
Dah.. hapana aisee.. hata kama kosa alifanya huyu marehem.. si kwa adhab hiyo. Babeki.. jamaa ana roho ya ajabu
 
Lakini kwanini wasiwahusishe tcra ili wajue sms ilitumwa kutokea mnara wa eneo gani, haiwi sahihi kwa 100% lakini inatoa clue ya kujua aliyeitumia simu mara ya mwisho alikua wapi.

Halafu kuna hilo swala la mume kutojulikana na ndugu wa mkewe, kwamba walikua hawajaoana? Kama hadi wamejua kua hua anapenda kujipima kwa hivyo vipimo means wanamjua.
Na mtu yuko Znz so uchunguzi ndiyo umesimama mpaka arudi? Akirudi akitoa alibi yenye nguvu mtakua mmepoteza muda gani hapa kati?

Usiwafundishe wataalam, nakuhakikishia wanafikiri zaidi ya hivyo unavyofikiri wewe! na watakuwa wameshaanza kuchukua hatua,
 
Back
Top Bottom