Kilosaone
JF-Expert Member
- May 3, 2015
- 407
- 219
Hii imetokea Leo Asubuhi ambapo nilimpeleka Mhudumu Ofisi yetu Benki ya NMB iliyopo eneo la Mkoani Mjini Kibaha ili aweze kuniwekea kiasi cha Shillingi Milioni 6 kwenye Akaunti yangu na kwa kuwa nilikuwa Nina shughuli nyingi Nikamuacha aendelee na Kuweka hizo pesa kwenye Akaunti.
Baada ya Dakika 45 nilipigiwa simu kuwa Binti yule ametapeliwa kiasi chote cha Pesa.
Mazingira ya Kutapeliwa yalikuwa hivi
Baada ya Yeye kujaza form na kukaa kwenye Foleni kuna Dada alikuja kumuuliza kama anajua sehemu ya kubadlishia Dora. Yeye akamjibu hajui. Baada ya Muda akaja Dada mwingine akamwambia amuelekeza sehemu ambapo kuna Benki nyingine. Akaanza kumuelekeza na katika hayo Mazungumzo akajikuta wale watu wanamtoa nje ya Bank ili awaelekeze vizuri. Nje akakutna na wadada wengine wawili ambapo walimzunguka na kuanza kumsikiliza jinsi anavyoelekeza na baadae akawafuta mpaka nje kabisa ya Benki na mwenyewe akiwa hajui kinachoendelea. Baada tu ya kuagana nao wale wadada akajikuta bahasha aliyoshika ya pesa ndani ina makaratasi na sio yenyewe. Ndipo alipogundua kuwa yupo nje ya Bank na tayari ametapeliwa. Tulipoenda Polisi Kituo cha Mailimoja tukakuta kesi zaidi ya Tano toka Asubuhi za Namna hii. Wengi wao wameibiwa kwa mfumo huu, na tukiwa tunaendelea na Maelezo akaja Dada naye akasema alipotoka tu Bank kuna mdada alimslimia kwa kumgusa alipofika mbele kidogo afungue pochi yake akakuta pochi sio yake na ndani kuna matambaa machafu. So Leo kibaha imekuwa ni Matatizo hayo tu. Kuna mtu niliongea naye Yeye alitoka mbeya kama Wiki moja iliyopita Akaniambia na huko pia kulikuwa na Matukio ya Namna hiyo.
Hivyo kuwa Makini Unapoingia Benki Mpendwa.
Kina #Mshana watadadavua zaidi inskuwaje.