TAHADHARI: Mvua kubwa Dar na mikoa karibu na bahari

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
614
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya tahadhari ya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia usiku wa tarehe 08-03-2016 hadi 09-03-2016.

Maeneo hayo ni pamoja na Dar es Salaam, visiwa vya Unguja na Pemba na mikoa yote iliyopo pwani ya Bahari ya Hindi ikiwamo Tanga, Mtwara na Lindi na pia mikoa ya Pwani na Morogoro.

IMG-20160308-WA0011-1.jpg
 
Yaani kwa miundombinu hii ya Dar hakuna amani kabisa
 
Dah!
Ishakuwa kero, mvua ikinyesha na usafiri shida na ukiupata ni wa kukanyagana na kupakana matope.
 
Huku kwetu tunaisubiri kwa hamu maana mazao karibu kukauka.
 
Naona itaanza mda simrefu maana huku juu kumeshafunga kwa sie wapande za manispaa ya temeke!!eee mwenyezi Mungu ipoze na iwe yakawaida aamen.
 
Kwenye zile chemba za posta haideri plaza.... kesho kitu inacheua
Kinondoni Mkwajuni naona wanaangalia mabondeni hawaoni walioziba njia za maji kama pale mtaa wa Mafere karibu na Shule ya Mwongozo ni balaa mvua ikinyesha nyumba za pale hujaa maji kama wako mabondeni lakini walioziba njia ya maji hawaguswi sijui kama Paul Makonda DC anajua ama la!!
 
Si unajua nchi hii wanasema all people are equal but some are more equal than others
 
Back
Top Bottom