Sio mlimani city pekee. Hata hapa Ubungo Plaza huyo kijana wa kipemba na kundi lake walianza kuiba site mirrors na magari ya watu. Bahati nzuri Ulinzi wa hapa ukawashtukia na kuweka ulinzi mkali. Mpaka leo tatizo hilo limekwisha kabisa. Tatizo la mlimani city ni la walinzi kushirikiana na wezi. Huyo kijana wa kipemba ni hatari sana. Infact ni wa kupiga risasi ya mguu awe kilema.
Mimi binafsi ninalilaumu jeshi la polisi kwa asilimia nyingi due to the following reasons:
Kumekuwa na wizi wa power windows, na vifaa mbali mbali vya magari and vimekuwa vikipelekwa maeneo yanayofahamika kabisa i.e. gerezani, mnadani, Buguruni and some places in Mwenge. Na jeshi la polisi limekuwa likishirikiana sana na hawa jamaa wanaoiba hivi vitu as kwa jinsi walivyo na comfo ya kuviuza peupe. Yaani utaibiwa vioo vya pembeni leo asubuhi, then mchana utavikuta gerezani vinauzwa kwenye maduka ya "used spares" and ukitoka hapo bila hata kushtuka, ukaenda polisi, mkirudi pale gerezani hamvikuti. Au hata kama ukiwa na information kuwa hv vitu vitakuwa gerezani, ukaenda then ukawashtukia halafu ukajifanya unapanic, kama ni wind screen hawakawii kuimwaga chini. Hawa wezi wamekuwa na kiburi, confidence ya ajabu katika nchi ambayo inasemekana kuwa na ulinzi wa jeshi la polisi. Si ajabu itafikia kipindi ukiibiwa vifaa vya gari ukaenda polisi kutoa taarifa, na kuambiwa, nenda gerezani/mnadani/buguruni utavikuta. Yaani tumekuwa tukinunua vifaa vyetu wenyewe and jeshi la polisi limekuwa likikaa kimya. Kova amekuwa akipiga tararira za wizi wa silaha na kusahau kuwa kuna wizi mwingine ambao umekuwa kama ka-falme ka kujitegemea. Hili limechangia sana kukua kwa wizi wa vifaa vya magari and no wonder hata kwa huu wizi wa magari.
Kwa miaka ya nyuma, ilikuwa ukiibiwa gari, linapelekwa Nairobi, au mkoa mwingine and mtu ulikuwa una nguvu ya kuanza kusaka gari ukitigemea kulikuta somewhere. Lakini siku hizi baada ya kuingozeka kwa maduka ya used spares, yaani ukiibiwa gari, after 2-3hours, ukawa hujaliona, yaani wewe nenda tu polisi, kaombe police report, and then uende moja kwa moja kwa Insurer, manake litakuwa limeshachinjwa siku nyingi na vifaa vimetawanywa hapa mjini.
Pia kuna soko jipya la vifaa vya wizi, ambalo nasikia liko Dodoma, and linafahamika hata na jeshi la polisi, but sioni any measures.
Kwa ufupi nashindwa kuelewa kuwa hawa kina Kova, Said Mwema, Wabunge, Mawaziri, Rais na wengineo, ni kwamba wanasubiria mpaka magari yao yaibiwe vifaa au..? (Kitu ambacho kwa hali ya kawaida ni ngumu). Then ndio tutegemee kusikia statement kuhusiana na huu "WIZI WA KIBABE"...???
Huyu jamaa wa kipemba naye, nimesikia sana wananchi wakimuongelea, but I doubt kama jeshi la polisi linamfuatilia. Mimi kwa wakati mwingine nimeanza kuhisi kuwa huu wizi wa vifaa vya magari na magari yenyewe unahusisha wakuu wa jeshi la polisi kwa kiasi kikubwa sana na ndio maana hata hatua kali hazichukuliwi.
Haya maduka ya used spares ni lazima yachunguzwe sana, and pia watu kama mpemba and wezi wa vifaa vya magari wafuatiliwe, and I tell you wizi wa magari na power windows utapungua sana.