Tahadhari: Mlimani city eneo hatari kwa usalama wa raia

na wale walinzi huwa wanafanya kazi gani ??
Hao walinzi nao ni choka mbaya. Wakati fulani mwaka jana waliwahi kugoma wakidai nyongeza ya mishahara, sidhani kama walipewa. nadhani ndio maana wameamua kushirikiana na wezi ili kujilipa kabisa
 
mimi nadhani muhimu ni kutoacha kadi kwenye gari, japo kuna wakati unaambiwa kadi zimeisha, at least utakua na cha ku complain and maybe kulipwa na kampuni ya ulinzi. maana sababu ya kutoa ile kadi ni usalama wa gari lako. wezi hawa wanashirikiana na walinzi. nimeshaona pale millenium tower mtu anaibiwa side mirror na mlinzi ndio analinda mwenyewe asitokee! so you can imagine. Mishahara midogo wanayolipwa ndio husababisha yote haya, hivyo wanafanya hivi kumkomoa tajiri. Pale ni muhimu waweke kamera kama Moeven Pick na Kempinski, itasaidia sana. sehemu nyeti kama hii kukosa camera hainiingii akilini.
 
polisi hawawezi kuhangaika hata siku moja wewe raia ukiibiwa kitu chochote. maana hawako kuangalia usalama wa raia, wako kwa maslahi yao wenyewe. wanajua mitandao yote ya wezi kwa sababu na wenyewe ni wezi. mkubwa akiibiwa gari litapatikana ndani ya saa 24, lakini wewe, sahau, sana sana utaambiwa uwasaidie, ulikiliona njiani uwape taarifa, na hiyo ni kama wataweza kuwahi, usishangae wakikuambia hawana usafiri. ndio polisi wabongo. kila wizi mkubwa unaotokea lazima uwahusishe, kuonyesha jinsi walivyo majambazi.
 
Back
Top Bottom