TAHADHARI KWA VIONGOZI WA KITETO.

TAHADHARI KWA VIONGOZI WA KITETO.

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
TAHADHARI KWA VIONGOZI WA KITETO.

Kwa mujibu wa hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi TUMAINI MAGESA kwenye kikao cha baraza la madiwani mwishoni mwa wiki.

Alisema inaonyesha migogoro ya ardhi Kiteto mara nyingi huibuka kipindi cha Kilimo

Kauli hii inatosha kabisa kujiweka sawa kwa kiongozi makini kuona namna ya kukabiliana na tatizo hillo

Sasa niwaombe viongozi wangu kuona haja ya kufanya hivyo kwani mpaka sasa kuna maeneo ambayo yanaonyesha mvua ikianza migogoro itaibuka na kuleta madhara

Maeneo hayo ni pamoja na Engusero Sidani, Endrango, Nhati ambako kuna maelekezo ya Serikali ambayo hayajafanyiwa kazi

Kwamba wakulima walikutwa kwenye maeneo wakifanya shughuli za Kilimo na kutakiwa wakubaliane na Serikali kuwekwa mabango kuwa ni maeneo ya malisho na hifadhi ili baadaye wapewe mengine waendelee na shuguli za Kilimo

Baada ya makubaliano na kuwekwa mabango wamegeukwa kuwa walivamia meneo hayo huku isijulikane hatma ya maisha yao ikoje mwaka huu kuhusu Kilimo

Binafsi nauona huu sio uungwana wanaifanyiwa kundi hili kwani kuna ulaghai uliofanywa na viongozi wa Serikali ya vijiji husika kuwa watatoa maeneo mbadala bila mafanikio zikiwa zimebaki siku chache wakulima waanze shughuli za kilimo

Sasa kwa hili nijuavyo kwakuwa maeneo ya namna hiyo ni mengi viongozi wa Kiteto mjiandae kurejea katika mgogoro tena kwani nionavyo suala hili haki haikutendeka

Ushauri wangu busara zitumike katika kuwahudumia wakulima na wafugaji hasa katika shughuli zao hizi za kujipatia kipato
 
Write your reply... Tunaisoma??
Wanaisoma??
Wayaaa
Wayaaaa
Tunasomana kifo cha mende chaliii
 
Back
Top Bottom