Tahadhari kwa mvua zinazoendelea nchi nzima ...

Tahadhari kwa mvua zinazoendelea nchi nzima ...

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Nimeota kuwa Tanzania itanyesha mvua kubwa itakayo haribu maeneo mengi sana. Nahisi huu ni mtazamo wangu kuwa Tanzania inatakiwa kujianda na mafuriko ya mvua ya hivi karibuni. Watanzania tuna mitazamo ya kizamani hadi likufike jambo ndio unajianda; hivi ni wangapi wametazama kwenye nchi kama Ufilipino hali ya hewa inavyowatafuna watu huko?

Kama umeona utashusha kwenye comment; yamkini Tanzania leo hii imesahau kuwa ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji. Kwanini watanzania msianze kujenga na kuboresha mitaro ya kupitisha maji? Mnatupa taka nyingi kwenye mitaro na mbaya zaidi lipo kundi la watu wanateka michanga kwenye makonde ya maji na hatuchukui hatua. Nasema hivi ukiona mwenzako ananyoa zako tia maji. Leo hii watu wanakata misitu uoto wa asili unaanza kupotea; Tanzania ya jana sio ya leo ila mtazamo wangu kama serikali itaanza kujikita kipiga marufuku utumiaji wa mbole za chemical ambayo hiyo ndio imeua mioto ya asili leo; Tanzania ingekuwa vyema. Huwezi kukuta uoto wa asili ukachanua kwenye sumu.

Natoa ushauri kwa sekita husika kama kweli mnataka kuiona Tanzania ya kesho pigeni marufuku chemical zinazo haribu uoto wa asili. Tunakwenda kwenye hatau mbaya sana kwani katika utafiti tunatambua kuwa mimea ndio chanzo cha mvua na kwa kuwa mimea inayokufa ni ya asili na kufanya mimea ya sumu kuchanua zaidi ile iliyopandwa kwa kutumia mbolea sumu; hakika mimea hiyo inakwenda kwanza kuua micro-organisms walio na faida kwa mimea na hivyo wapo wadudu watakimbia kutoka ardhini na kuanza kula mazao ya wakulima. Mtaangaika kutafuta dawa ya kua wadudu lakini ikiwa ninyi ndio mnapanda mbole ya sumu kwenye ardhi wadudu wanakimbia nje ambapo wanaleta athali kisha mnajiuliza nani mchawi; wakati wenyewe ndio wachawi.

Jambo la pili mimea hiyo kwa kuwa ndio chanzo cha mvua 100% transp inayofanyika katika circle ya utungaji wa mvua utashuhudia mvua zinazonyeshea Tanzania zitaanza kuwa za majanga makubwa sana. Narudi Tanzania msipo ziba ufa mtajenga ukuta kwani njaa na mafuriko yanakuja kesho kutwa uwe tayari katika hili.

Hii ni ndoto tu!
 
Siyo umeota! Moderator Njoo uunganishe hii thread na ile ya mamlaka ya hali ya hewa.
 
Back
Top Bottom