Tahadhari! Flashlight App sio salama

ethicx

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
311
Reaction score
127

​

Habari zenu wadau, taarifa ni kwamba kama ume install Flashlight App yoyote kwenye smartphone yako au tablet upo katika hatari ya kuchukuliwa data zako muhimu.

Nikwamba most Flashlight App unapo install ina install na malware ambayo inamwezesha developer wa App hiyo kuiba taarifa zako muhimu na kuziuza kwa third party entities kwenye kifaa chako, mfano:-

  1. Kuwasha GPS na kujua ulipo bila wewe mwenyewe kujua.
  2. Kusoma SMS na emails zako
  3. Kuiba credentials zako wakati unafanya manunuzi online
  4. Kuiba contacts
  5. Kuiba call records
Unachotakiwa kufanya ni UNISTALL na backup data zako kisha fanya FACTORY reset. Ukitaka ku install flash App yoyote angalia size yake <900kb na haina permission nyingi. Pia na recommend tumia snoopWall App au angalia Flashlight App ambayo ni opensource badala ya ANT-VIRUS apps.

Chief Engineer of Computer Security Infrastructure Systems.
 
Hahahhahaaaa mimi hata wakiiba na kusoma sms zangu wanajisumbua maana watakuta benki kunasoma zero kila siku, SMS nyingi ni za mademu na za kupigwa vizinga. Labda wazichukue wakatengenezeee story

Hahahaha mbavu zangu mie


Watu wengi huwa hawaelewi umuhimu wa faragha(Privacy) katika vyombo vyao vya mawasiliano ila kama mtaendelea kuwepo duniani mtaelewa maana yake. Hata hapa JF kuna page ya Privacy Policy na inawezekana zaidi ya 90% wanajukwaa hawajawahi kuipitia,then tunajiita wasomi tunaoenda sambamba na teknohama.
 
Je hizi flash light app ambazo zinakuja installed ktk sim km app za kawaida km s4 nazo majanga?
 
Je hizi flash light app ambazo zinakuja installed ktk sim km app za kawaida km s4 nazo majanga?

Hapana nazungumzia zile ambazo una install mwenyewe kutoka playstore kwa ridhaa yako.
 
Mpwa wangu naelewa sana unachokisema but my point is, kama mtu anataka kupata taarifa zako atatafuta namna yoyote ile nyingine azipate tu. N akwa level yetu ya Teknolojia hatuwezi kushindana nao. Ni hicho tu ila kama Baba asingeomba simu akaomba teknolojia basi walau tungeweza kuelewa haya mambo. lakini pia hakuna mtu ambaye bni expert kwa kila kitu, naweza kuwa expert kwenye field hii lakini pia nikawa kilaza kwenye Teknohama, bado hainiondolei maana ya kuwa msomi
 


Umenielewa vibaya mkuu, angalia kwenye rangi nyekundu hapo. Nakubali utakua msomi bali sio unaeendana sambamba na teknohama. Na kuhusu expertise katika maswala ya mawasiliano usitumie neno HATUWEZI sema SIWEZI kushindananao. Hayo mambo tunayoyaona kwenye MOVIES/SERIES kuhusu teknohama usifikiri hata kidogo kuwa yanawezekana in real world situation.
 
Hahahhahaaaa mimi hata wakiiba na kusoma sms zangu wanajisumbua maana watakuta benki kunasoma zero kila siku, SMS nyingi ni za mademu na za kupigwa vizinga. Labda wazichukue wakatengenezeee story

Mkuu umenivunja mbavu sana, ila kiukweli kwa waboongo wengi hakuna data za muhimu kuiba, ni watu wachache sana ambao huweka credential data kwenye simu zao, mi ukiniibia simu yangu nitajuatia kupoteza simu lakini sio data muhimu
 
Asante kwa taarifa!
.
.
kibongo bongo labda wa si-ra ndo ana data muhimu!
 
Hahahhahaaaa mimi hata wakiiba na kusoma sms zangu wanajisumbua maana watakuta benki kunasoma zero kila siku, SMS nyingi ni za mademu na za kupigwa vizinga. Labda wazichukue wakatengenezeee story

hahaha mpwa una vituko
 
Mpwa hizi LIKES huko kwako huoni hio button? Hahahahaaa just kidding bhana
hahaha mpwa una vituko
JF Senior Expert MemberArray


Join Date : 3rd November 2013
Location : Dar es salaam
Posts : 11,390
Rep Power : 298523662
Likes Received6065
Likes Given17​
​
 

mpwa mi natumia wapsite siwezi kugonga like lols
 
hii iasue ni ya zamani na google mwenyewe anaruhusu. asilimia 90 ya apps za bure maaarufu ni malware mule playstore.

cha muhimu uwe mjanja kuangalia permision. mfano flashlight app inatakiwa iombe permission ya camera tu maana ndio flash ilipo. ila unakuta inaomba sms, app history, location nk.

halafu mtu unaweza ukajiona wewe huna cha kuibiwa ila wakipata data za nchi nzima ujue wanawafanya nyie ndio dump la takataka maana wanajua kila mnachokipenda na msichokipenda.

mnafkiri kuna mchina alikuja akafanya research waafrica wanapenda dawa za kuongeza makalio? tunatoa data wenyewe tena bila kujijua. wanatujua ndani hadi nje vitu tunavyopenda, vitu tunavyoogopa, ndio maana kila wanachofanya kwetu kinahit na vyetu vinaflop
 
Hahahhahaaaa mimi hata wakiiba na kusoma sms zangu wanajisumbua maana watakuta benki kunasoma zero kila siku, SMS nyingi ni za mademu na za kupigwa vizinga. Labda wazichukue wakatengenezeee story

Ndugu issue ya security ni muhimu sanA hata kama unafikiri kwenye kifaa chako kama computer au simu huna kitu cha muhimu, hicho kisicho na umuhimu kwako kinaweza kua thamani kubwa sana kwa mwingine.
mfano contacts zako za simu, favourite calls, picha zako na rafiki zako zinaweza kua na faida kubwa kwa matapeli.
Mtoa mada amegusia suala muhimu sana la privacy.
Kingine hakikisha kifaa chako kina security (pin or security code ) ni muhimu sana kujikinga na malware tunaoishi nao (physical malware ) mfano mfanyakazi mwenzako au mtu wa karibu anaweza kua na madhara makubwa kuliko hata viruses tunaowagopa na kuwanunulia antivirus za garama lakin tukiacha computer zetu on bila hata password mtu anajichukulia data nakuondoka zake bila hata ww kujua
mwisho wa siku unakua exposed kwa kila hatua unayoipiga
 

Kweli watanzania wengi hatufahamu maana ya faragha,,,,,anaesema hivyo anahitaji shule ya kutosha &#128518;&#128518;&#128518;&#128518;&#128518;&#128518;
 
Uje baadae nikusaidie ku-download Apps ya JF, ila uje kimya usiwaambie watu wengine, tukutane pale pale pa juzi

hahaha app ya jf ninayo mpwa ila inazingua naitumia kupata notification tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…