gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 814
- 1,490
NIMEIONA MAHALI NIKAONA TUISHEE WOTE ILI TUWE AWARE!!
Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo Wapka.mobi
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayo inamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya
Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa
Mtanzania yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulipa ada ya shilingi 37,000/=.
BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
29/5/2013