Tahadhari: Epuka kutumia simu ukiwa Barabarani

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,980
Reaction score
4,284
Wasalaam,

Wajumbe bila shaka mpo salama. Ni muda mrefu sijaandika chochote hapa kijiweni.

Leo nataka kurudia tu kile ambacho mara nyingi kimekuwa kikisisitizwa juu ya matumizi ya simu kwa madereva wakiwa wanaendesha.

Vijana wengi sasa wanamiliki magari kwa kuwa imekuwa nafuu kumiliki gari. Showrooms zipo kila mahali, wauza magari chakavu nao ni wengi, na bei pia imekuwa himilivu. Kama huna pesa taslimu, basi kuna wanaokopesha.

Matokeo yake ni kuwa wamiliki binafsi wa magari wameongezeka hapa nchini, hasa kwenye majiji makubwa, huku Dar es Salaam ikiwa kinara kwenye idadi ya magari mengi.

Kumiliki gari ni jambo moja, lakini kuzingatia kanuni za usalama barabarani ni jambo lingine kabisa.

Kwa kuwa wengi wa madereva wapya wanapata leseni kupitia mlango wa nyuma bila kupata mafunzo ya udereva na kufundishwa usalama barabarani, ni kawaida kabisa kukuta dereva yupo barabarani na hajui kabisa taratibu za udereva.

Leo nitaongelea matumizi ya simu barabarani kwa madereva, na wengine wameenda mbali zaidi mpaka wanachati kabisa huku wakiwa barabarani.

Binafsi nimeshuhudia matukio matatu ambayo yalisababisha ajali kwa sababu dereva alikuwa akitumia simu huku akiwa anaendesha.

Tukio la kwanza:
Mwaka 2018, asubuhi nikiwa natoka Mwenge kuelekea Posta, pale kwenye taa za Morocco, dereva aliyekuwa upande wa kukunja kwenda Magomeni alikuwa anachati huku anaendesha. Tulipokuwa tunakaribia, taa nyekundu ikawaka, sisi tukasimama, yeye akaendelea kuendesha. Wakati huo magari yanayotoka Morocco stendi kuelekea Msasani yalikuwa yanapita. Akaligonga daladala la G/Mboto – Msasani ubavuni. Ni ajali ambayo sisi wa pembeni tuliona kabisa jamaa ameitafuta, maana alikuwa bize na simu.

Tukio la pili:
Mwaka 2023, barabara ya Buza - Tandika pale reli inapovuka barabara; jamaa akiwa na Nissan X-Trail anatokea Tandika kwenda Buza. Wakati treni imeshapiga honi, yeye anazungumza na simu, akakatisha reli, treni ikampita naye.

Tukio la tatu:
Mwaka 2025, hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, eneo la parking – jamaa anatoa gari huku macho yapo kwenye keypad ya simu, anachat. Akarudi nyuma bila tahadhari, akagonga gari nyingine. Mashahidi wakaja juu kuwa walimuona alikuwa anachati.

Lengo langu ni kukupa tahadhari wewe dereva ambaye unadhani kwamba unaweza kufanya chochote ukiwa unaendesha gari.

Kama ni lazima sana kutumia simu, basi uwe na kifaa cha bluetooth – na hii ni kwa ajili ya kupokea tu. Japokuwa pia ina madhara, maana unaweza kupewa habari mbaya ukiwa kwenye spidi ya 120 kwenye kipande cha Ubena Zomozi au Kabuku – Segera, ukaachia usukani.

Chatting epuka kabisa. Kama ni muhimu sana kupeleka ujumbe, tafuta sehemu salama, egesha gari, kisha ufanye hizo chatting.

Epuka ajali zisizo za lazima. Okoa mali na uhai wako na wa wengineo.

Kaka yenu.
 
Don't text and drive,
Your life is worth more than any price that can be paid,
So,don't do it,
Stay safe.
 
Asante kwa somo zuri...nami mdogo wangu aligonga gari la kifahari la Ubalozi X,akavunja taa za nyuma akiwa anachat, palikuwa hapatoshi😀
 
Tatizo ni ULIMBUKENI TU.
Ulishawahi kumuona MZUNGU anachati barabarani? Lini na wapi???
 
Back
Top Bottom