kzba
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,355
- 790
Kwa wale wenzangu na mimi tuliojaliwa kupata kausafiri ka miguu minne(magari) tafadhali ukiwa unatoka Morogoro kuelekea Chalinze kama unaenda Dar na kwingineko ukikuta basi limekutangulia mbele yako maeneo ambayo wewe unaamini ni ya salama ukalipita inakula kwako.
Hawa ndugu zetu trafiki kuna kamera wamefunga kila mahali za spidi ambapo ni wewe huwezi dhania na kudharau kwa kuona kibao cha 50 au no overtaking ww ukajiona mjanja na mambio yako usizingatie alama za sehemu husika kwa taarifa yako utapigwa faini mpaka ukome.
Jamaa hawataki rushwa hata uwaombe vipi, maana wanaogopa zile kamera mwisho wa siku mkuu wao anazitrack kujua ni magari mangapi yamevunja utaratibu na hatua gani wamechukua dhidi yao.
Mimi ni mhanga wa hilo jana nilikuwa natoka Dom to Dar yakanikuta hayo na wamechukua faini yangu kiulaini maana nimekuta hadi ambulance liko wanalipiga fain dadadeki.
Nilichogundua watu wa mabasi wanajua hasa ya Abood kuwa sehemu gani ni vimeo.