Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,413
- 31,403
Ni mmoja wa wale wanaotaka mabadiliko, lakini si mabadiliko tu, bali mabadiliko ya kweli na ya kudumu.Kuna watu wanataka mabadiliko lakini pia wana watu WAO mahsusi wanataka wayalete hayo mabadiliko, tofauti na hapo watayapinga hayo mabadiliko. Natumai mkuu Nguruvi sio kati ya watu hao.
Ni mapema sana kumuita Magufuli mkombozi au kumpa sifa za kiongozi ambaye ameshafanikiwa. Ila ndani ya muda mfupi kwa mtu mwenye tamaa ya mabadiliko atampa kitu kinaitwa "benefit of doubt". Ni kweli unachosema kuhusu mfumo, lakini pia ni kweli huo mfumo unaesema hauwezi kuja ndani ya mwezi mmoja wa kuwa madarakani. Hata baraza lake ya mawaziri hajatangaza unategemea tayari mfumo utakuwa umebadilika? Tena una mtabiria na KUFELI juu?! Labda anaweza kuja badilika na asimalize kama alivyo anza, lakini kama unataka kuzungumza haki, kwa kipindi hiki kifupi ameonesha yeye anataka kuwa raisi wa aina gani. Na kwa hilo mimi binafsi nampa benefit of doubt.
Labda kwa maono yako, ili abadili huo mfumo unausema ndani ya kipindi hiki kifupi alikuwa anatakiwa amesha tekeleza jambo gani yeye kama raisi? Je alitakiwa asifanye haya aliyoyafanya mpaka sasa mpaka huo mfumo mpya utakapo kuwa tayari? Je hakuna uwezekano wa yeye kufanya aliyoyafanya mpaka sasa na bado akaja WEZESHA kupatikana kwa huo mfumo ndani ya miaka mitano ya uongozi wake?
Si kweli kuwa hatuhitaji kufukuza wakurugenzi na makamishna. Katika huo mfumo unauosema hii inaitwa ACCOUNTABILITY. Hakuna mfumo utakao kuhakikishia hutapata mkuregenzi ambaye pamoja na kuwa CV inayomuonesha kuwa ni competent ikakupa guarantee hatakuja kufanya makanjanja. Kufukuza na baadae kuacha sheria ichukue mkondo wake huko ndio kunaitwa KUMUAJIBISHA mtu. Hilo sio suala la kimfumo peke yake, ni suala UTENDAJI makini. Mfumo unaweza kuwa mzuri tu ila kama kila anaetakiwa kuhakikisha huo mfumo unafanya kazi akikosa umakini na uzalendo katika utendaji wake huo mfumo hauwezi kufanya kazi.
Najua tumeng'atwa na nyoka, unyasi unatutatiza lakini sisi bado ni taifa changa na tuna kila sababu ya kuwa Optimistic. Hebu tusubiri walau serikali yake ipitishe bajeti ya kwanza halafu tuone hakuna dalili ya huo unaitwa mfumo kubadilika then tuje hapa kuongea ila kwa sasa haya maandiko yetu na malalamiko yetu ni PREMATURE na kuwa wengine watakuwa na haki ya kuyaona yako FULL OF PREJUDICE.
#BEINGOPTIMISTIC #CHANGETANZANIA
Si mtu wa kuchora mstari kwa kutumia nukta moja. Ninataka kuona ramani nzima na points between ili nichore mstari.
So far hakuna ramani hakuna sketch diagram bali ni political stunt.
Nitasimama kwa hilo hata kama nitapewa label ya uzezeta, zumbukuku n.k. Ninaamini katika muda mfupi na mrefu
Umesema vema kabisa, na mfano wako unaweza kuonekana vema katika uzi wa leo wa The Boss
The Boss ameonyesha jinsi bodi za TRA zilivyo na matatizo katika uteuzi wake
Kilichofanyika kwa bosi wa TRA ni sahihi, lakini hakijawa solution kama tunavyoaminishwa na Magufulimania zealots
Wengi wanashindwa kuelewa kuwa kuwajibika hakuwezi kuwa mabadiliko.
Kama tunampa benefit of doubt ya kuwajibika sina tatizo, lakini hilo haliwezi kuwa mabadiliko.
Lakini pia kuna mwingiliano kati ya kuwajibika na kutengeneza mfumo.
Tumeona DC akasweka watu ndani bila sababu na kukiuka haki za binadamu kwa kutowafikisha mbele ya sheria, kwa kutotumia sheria za kazi n.k. Ni kwasababu hakuna mfumo bali kutegemea nani yupo magogoni
Tumeona anafukuza watu TRA , lakini je, amejiuliza kwanini Bosi wa TRA alikuwa na majina na hakuyafanyika kazi?
Je, DCI, DPP, PCCB walikuwa wapi? Mbona hakuna kuwajibishwa kwa muda mfupi sambamba na TRA?
Hili tu linaonyesha kuwa hakuna ramani ya kutengeneza mabadiliko.
Kilcihopo ni kukurupuka ndiyo maana ninasema kwa mwendo alio nao, kuwajibika pekee kutapeleka KUFELI.
Timu kama ya Brazili inatandaza kandanda safi si kwasababu wachezaji wake ni w wenye maguvu bali wanatumia maarifa kuwashinda wenye maguvu
Anachofanya sasa hivi ni kutuonyesha mapungufu ya mfumo yanayopelekea matatizo yanayoibuliwa.
Tumpe benefit of doubt ya kuweka wazi uozo wa mtangulizi wake, lakini hayo si MABADILIKO kama tunavyoaminishwa.
Ni majukumu yake ya kuwajibika. Mabadiliko tutayaona pale atakapobadili mfumo na kuja na kitu tofauti
Mabadiliko ya kweli ni kufumua mfumo wa kutegemea mtu mmoja, na kumuacha Rais atazame nchi kwa ujumla wake si kukimbizana na vitanda na MRI.
Kama bodi ya Muhimbili imefeli, mkurugenzi amefeli na wote waliteuliwa na Rais aliyeondoka, ni wazi kwa mfumo huo huo naye atafeli. Uteuzi wake na kutoa bilioni 3 hapo hapo unaonyesha tatizo si Mkurugenzi, bali mfumo uliopelekea mkurugenzi kushindwa. Je alifanya utafiti kubaini tatizo lilianzaje na nani anahusika? Ikiwa hazina hawakutoa pesa, huoni kama tatizo ni pana kuliko mkurugenzi
Muhimbili ili feli kwasababu mfumo wa kupata watu makini unategemea mtu
Tunataka mfumo utakaomwezesha yeye kusimama na kuangalia 'muhimbili' zote nchini na si MRI mmoja
Hilo litawezekana ikiwa tu tutakuwa na mifumo inayomwajibisha kila mmoja wetu. Kwasasa mtu mmoja ndiye mfumo
Last edited by a moderator: