Tafsiri potofu ya agizo la Rais Samia kuhusu kodi itaigharimu Serikali

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Rais Samia kwa nia njema kabisa ametaka TRA waache mabavu kukusanya kodi. Ila kwa uzoefu na hulka ya binadamu huwa hawapendi kulipa kodi. Naam kodi ikusanywe kwa mujibu wa sheria bila uonevu ila kuna haya ya kuangaliwa laa sivyo serikali itakosa zaidi;

Mosi, kukubali hadharani kuwa miezi mitano au sita ijayo mapato ya serikali yatashuka ni ujumbe kwa TRA kuwa wasifanye jitihada kukusanya mapato.Sijajua serikali itafidia vipi upungufu huu wa makusanyo.

Pili, ni hulka ya binadamu kutopenda kulipa kodi sasa kuamini kuwa mfanyabiashara atatoa taarifa zake sahihi kwa TRA hapa kuna shida na hii inatoa mwanya mkubwa kwa watumishi wa TRA na Wafanyabiashara kuamua ngapi ziende Serikalini.

Nimalize kwa kusema kuwa maagizo ya Rais Samia kuhusu kodi yamepata tafsiri potofu na kama serikali isiporekebisha yale malengo ya kukusanya trilioni mbili kila mwezi yatabaki kama matamanio.
 
Acheni roho mbaya nyie mliokuwa mnashangilia wafanyabiashara kufilisiwa kwa dhuluma tu!

Rais Samia hajawaambia TRA wasikusanye kodi, ila kawaagiza wakusanye kodi kwa haki siyo kudhulumu watu!

Tatizo kuna watu ni Saddist kama mtoa mada ambaye anafurahi kuona watu wakifilisiwa wakidhulumiwa wakiteseka! Acha watu walipe kodi kwa haki na siyo kwa mateso na unyanganyi.

Wenye akili wanamuelewa mama Samia, ila walio zoea kulamba viatu ndo mnateseka hiyo awamu ilishapita tayari;

Mlizoea kula kwa dhuluma sasa fanyeni kazi kwa haki!
 
Acheni roho mbaya nyie mliokuwa mnashangilia wafanya biashara kufilisiwa kwa dhuluma tu!

Rais Samia hajawaambia TRA wasikusanye kodi, ila kawaagiza wakusanye kodi kwa haki siyo kudhulumu watu!...
Amini nakuambia ni ukabila na udini unawasumbua wanashindwa kusema.... kuna watu wana kasumba ya kuamini kuna maraisi wa dini fulani huleta ruksa nyingi na wegine kazi yao kubana.

Hawa watu wanapenda sana viongozi sadist..hawapendi kuona watu wana furaha...akili zao za kimaskini sana
 
Back
Top Bottom