Tafiti ya CCM imempa Dkt Shein ushindi wa 60 %

Tafiti ya CCM imempa Dkt Shein ushindi wa 60 %

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,783
Reaction score
9,709
Zanzibar. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema utafiti kilioufanya tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unaonesha kuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Dk Ali Mohamed Shein anaongoza kwa zaidi ya asilimia 60 dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

Akizungumza kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Kisiwa Ndui leo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai amesema matokeo hayo yametokana na kazi nzuri aliyoifanya Dk Shein katika miaka mitano ya awamu ya kwanza ya uongozi wake.

“Tathmini imeonyesha kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM anakubalika zaidi kuliko wagombea wote wanaoshiriki kwenye uchaguzi huu na kwa kukisia tayari anaongoza kwa zaidi ya asilimia 60,” amesema Vuai

Ameongeza kuwa tathmini hiyo inaonyesha kuwa Dk Shein anaongoza kutokana na udhaifu wa mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad anayegombea kwa mara ya tano bila mafanikio.

Vuai amesema kuwa Dk Shein amewapiku wagombea wengine kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusimamia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho kwa asilimia kubwa.

Tathmini hiyo inaonyesha kuwa CCM inatarajia kupata kura nyingi kutoka Pemba ambako kwa muda mrefu kumekuwa ni ngome ya CUF.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM ameeleza kuwa wana CCM katika kisiwa hicho wamekua kidemokrasia hivyo uchaguzi huu hawatatishwa kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizotangulia.
Source Mwananchi.
 
Ccm Zanzibar pamoja na wizi wote tangu uchaguzi wa 1995 haijapata ushindi zaidi ya 54% na hawajapata ata kiti kimoja Pemba since 1995.Sasa mwaka huu Maalim Seif anagombea akiwa Makamu wa Raisi hii ina maana ule wizi na kutumia polisi kumsumbua kama kipindi kile cha nyuma utapungua sana,katiba ya wananchi kukataliwa na Ccm kumeleta kuchukiwa zaidi kwa Ccm Zanzibar pamoja na wenye nguvu wengi waliokuwa Ccm kuingia Cuf kama mzee Moyo na Mansoor aliyekuwa waziri Zanzibar, ujio wa Lowassa na Ukawa umemwongezea nguvu zaidi Seif maana Unguja si ngome tena ya Ccm.Maalim Seif atashinda kwa zaidi ya 59%.CCM OUT
 
CCM bhana, wanajua kweli mchezo wa kujitekenya na kucheka wenyewe!
 
ccm hata asilimia 20 zenj haijawahi kupata na haitatokea kupata.
 
Back
Top Bottom