real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Chama wa Mawakala wa Forodha nchini Tanzania (TAFFA) kimeitaka serikali ichukue hatua za haraka kukabiliana na madhara ya kiuchumi yanayoweza kuletwa na kupungua kwa mizigo inayopitia katika bandari mbali mbali nchini.
Akizungumza na wanahabari, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga alidai kuwa mojawapo ya sababu za kupungua kwa mizigo bandarini ni matumizi ya sheria ambazo sio rafiki kwa ustawi wa biashara na zinazokimbiza wateja hasa wale wanaotoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia, Rwanda, Burundi na Malawi.
“Sisi kama wadau hali hii tulishaiona takribani miaka mitatu iliyopita na tukatoa angalizo kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kukabiliana na hali hiyo….lakini badala yake, serikali wakaja na sharia ya ushuru wa VAT kwa mizigo inayokwenda nje ya nchi na hivyo kuwakimbiza wateja,” amesema Ngatunga.
Kwa mujibu wa Bw. Ngatunga, wafanyabiashara kutoka nchi za DRC, Zambia na Malawi hivi sasa wameanza kutumia bandari za Beira nchini Mozambique, Welvis Bay nchini Angola, Cape Town Afrika Kusini na nyinginezo kutokana na mazingira rafiki ya kibiashara yaliyopo katika nchi hizo.
Ngatunga amefafanua kuwa ushahidi unaonekana hasa katika maeneo ya mipakani na kwamba kupungua kwa mizigo kumeathiri takribani ajira elfu kumi zinazotokana na mnyororo mzima wa usafirishaji mizigo kati ya bandari ya Dar es Salaam na maeneo ya mipakani na kutaja biashara zilizoathirika kuwa ni wauzaji wa mafuta ya magari, wauza chakula maarufu kama Mama Ntilie, wamiliki wa nyumba za kulala wageni kutokana na kupungua kwa wageni wanaolala katika nyumba hizo.
Chanzo: East Africa TV