Bila ya hawa ambao wewe unawaita wavuta bange, haki zetu nyingi zitavunjwa na tutacharazwa viboko hazarani. Bila ya hawa tusingepata fedha za rada, bila ya hawa Escrow, RichMond, green finance,........ Nk nk visingejulikana na tungeliwa mpaka damu yetu. Hawa ndio wanaowatetea wakulima, wavuvi, wafanyakazi, wafanya biashara nk nk. Hii haina maana chama tawala CCM ni kibaya la hasha. Bali madaraka yanalevya mno bila ya kuwa na chama angalizi wakulima wataumizwa, wafanyakazi watateswa, wafanya biashara watatozwa kodi isio stahili yao, raia tutaswagwa bila kujua tunakopelekwa nk nk. Vyama hivi pinzani hutumia muda wao mwingi vikifanya tafiti, uchunguzi, ushauri na kutoa madokezo penye hatari. Mfano mzuri ni hivi karibuni mh Heche amesema bungeni ana ushahidi mh Rais kadanganywa kwenye suala la e-passport. Bila ya Heche yasingejulikana.
Japo kwa hali ilivyo navishauri vyama hivi VISIANDAMANE kwa sababu hali haitabiriki.
WASIANDAMANE kwa sababu mwisho wake ni makovu ambayo kuyaponya ni ngumu.