Tafakuri: Whistleblowers wa awamu ya Tano ndio wamekuwa wacheza samba ya awamu ya Sita

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,705
4,739
Mafupi marefu, awamu ya JPM kulikuwa na wafia upingaji na wanamatusi wa mhimili wa serikali kupitia mitandao ya kijamii wakiongozwa na mchambuzi kigogo 2014 kule Tweeter na Mange mchambaji kule Instagram kabla hajatulizwa akatulia. Hawa waliongoza na kuhamasisha hadi maandamano mitandaoni na katika ardhi waishizo. Well and Good We called it Democracy!

But Ghafla bin Vuu wote wameibukia kuwa wacheza samba wa awamu ile ile ikiitwa ya sita ambayo Samia Suluhu alikua VP na mmoja wa wa serikali ile ile. Mwingine kasema kama akirudi 2025 basi atakuja kumpigia kampeni Samia Suluhu.

Mwingine kagombania vikumbo huko kupiga picha na Mh. Rais, na kuweka maneno ya sifa kedekede na mamlaka ile ile inawaangalia na kuona ni sifa, well and good.

Tafakuri: Hawa watu we all know walikua wanted badly na regime iliyopita na sasa ni sugar coat na mamlaka inawa pet pet, na wakati ule walikua wanaongoza kuvujisha siri za awamu ya Tano na sasa hivi hakuna siri zinazovuja! So, which is which and who is who!?

Ushauri: Mamlaka ni mamlaka mkiacha kiraka cha mamlaka kiwazibie matako ya suruwali ya fundi seremala mtakuja kujuta mbeleni. Hata Mbeleko Huchanika.
 
Back
Top Bottom