TAFAKURI: Umeshawahi kujiuliza hili?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,479
Reaction score
40,120
Waungwana,
Inawezekana Watanzania wengi wanatembea kwa kupapasa-papasa kama wapo kizani. Tena hili linawahusu hata wasomi wetu wengi na wanasiasa wa pande zote mbili yaani tawala na shindani.

Tangu nchi iamue kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kumekuwa na maigizo na miendendo ya kifutuhi kwenye mfumo wa utawala wa nchi hii. Sheria ya vyama vingi ilipopitishwa kuliambatana na mabadiliko (viraka) ya katiba ili iendane na mfumo tulioukurupukia kabla ya kuutathmini na kujenga misingi yake.

Mojawapo ya sheria zilizorekebishwa ni kutenganisha utumishi wa umma na siasa ambapo waajiriwa wa serikali hawapaswi kujiingiza kwenye movements za kisiasa. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama walitenganishwa kabisa na siasa hadi kupigwa marufuku kujiunga na chama ama kundi lolote la siasa. Haya ni baadhi tu lakini kinachoendelea ni maigizo tena ya kitoto mno.

Leo mtu kama Chenge ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, anasimama na kutumia akili, nguvu na elimu yake kupiga siasa za hovyo. Haiyumkiniki hata mrithi wake Mwanyika na sasa Werema wamewahi kutoa kauli zinazoashiria bila shaka yeyote unazi wao wa kisiasa hasa ukichukulia wao ni watumishi wa umma ambao hawapaswi kuwa na maslahi ya kisiasa. Tukumbuke tukio la mmoja wa wagombea wa jimbo la Mhe. Tibaijuka katika kura za maoni alikuwa ni Alfred Tibaigana ambaye alitoka kustaafu muda mfupi nafasi ya RPC wa Dar lakini alirusha karata yake kutaka kuingia siasa huku akiacha maswali lukuki nyuma, vivyo hivyo ilitokea kwa Mboma (Mkuu wa majeshi mstaafu). Ikumbukwe CCM na vyama vingine wamekuwa na hulka ya kutoa kadi kwa wanachama paywa kwa mbwembwe kama ilivyofanyika kwa vijana wale wasanii kule Mbeya wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM na kadhalika. Lakini Hakujawahi tokea siku ambayo watu kama Mahita, Mboma, Tibaigana, Fabian Massawe na wengineo walipewa kadi zao na rekodi kuwekwa hadharani.

Hoja yangu hapa ni kwamba, wanasiasa wengi tulionao leo madarakani ni wale ambao ktk utendaji wao walikiuka sheria za nchi kwa kuchanganya siasa na utumishi wa umma hususani ulinzi na usalama huku wakiwa na kadi za chama mfukoni ambapo zimewasaidia kupata ulaji (kama wanavyouita wenyewe) kwenye nafasi za dhamana. Hii inapelekea tija kutozingatiwa kwenye utendaji wa maafisa wengi wa serikali ambapo wanafanya hivyo kukipendezesha chama zaidi ya job descriptions zao.

Tujiulize, kwa utendaji upi uliompatia Kanali Shimbo nafasi ya kuiwakilisha nchi kama Balozi hasa ukichukulia matamko yake dhidi ya umma wakati wa Uchaguzi Mkuu 2010 ambapo alitoa vitisho vya kijeshi kwa wapiga kura huku akilazimisha watu kukubali matokeo huku akijua uchaguzi hautakuwa Huru na Haki kutokana na bias ya uteuzi wa wajumbe wa Tume yetu ya Uchaguzi.

Tujiulize sasa TIJA ya yote haya na mengieyo kwa mustakabali wa nchi yetu hasa tukiamini kwamba kiongozi na Afisa wa serikali lazima wawe mstari wa mbele katika kushika na kuheshimu sheria za nchi.

Inawezekana kwa UPOFU tu watu hawalioni hili na wanakurupukia sheria ambazo zitawasaidia kuingia madarakani wale matunda ya uhuru.

Kikwazo kikubwa ni hawa marais tunaowapata siku hizi ambao hawana soni wala uoga mbele ya sheria. Wanafanya lolote hata kuweka jamaa zao na makada kwenye nafasi ambazo hawana sifa nazo na kuwaacha Watanzania wenye sifa na uwezo nje.
 
Ndugu yangu mtawala yeyote hupenda atawale milele.

Wegi katika viongozi wetu hawaaminiki katika matamshi yao sababu hata wenyewe huwa hawaamini wanachokitamka.

Mifano yako ni usahihi wa ghilba zinazotutesa Watanzania.

Tuko radhi kujenga Mahekalu yenye kuta ndefu bila kujali kuwa kinyesi kitakuwa kimetapakaa hadi katika mageti ya mahekalu yetu.

kazi kwetu kuamka.
 
Msanii viongozi wetu hawakuwa tayari na mfumo wa vyama vingi na pili hawakujua kama utakubalika kwa asilimia hii.Na kwa sababu ya uwoga wao ndiyo maana chama tawala kinatumia zaidi polisi na jeshi ili kuwabana watanzania,na kwa vile pesa ndiyo imekuwa fimbo yao kuua kwao siyo tatizo ili mradi walichokitaka kimekuwa.Lakini wanasema haiwezekani kuwadanganya watu wote kwa wakati wote.
 
Kweli kabisa mkuu.

Ndo maana fisadi haoni soni kukausha hazina ya nchi kwa sababu anajua kesho atakuwa ndiye mtoa maamuzi.

Hadaa hii ina kiini chake ambacho ni RUSHWA ya madaraka. Watu wamehaidiwa nafasi nzuri kisiasa ndo maana hata ktk utendaji wao wa kitaaluma wanaweka nchi kando na kushika bendera za chama kokote waendako. Angalia namna makanali na makapteni waliojazana kwenye siasa ndipo ujue ujinga ulipoanzia.

Angalia Majaji wastaafu wanavyopewa ulaji kwenye asasi za serikali zinazokalia haki za msingi za raia kama vile Tume ya Uchaguzi, Msajili wa vyama, Tume ya Haki za binaadam na kadhalika.
 
Kinachostua ni namna ambavyo jamii imekuwa inahadaika kwa urahisi mno.

Hata hawa tunaowaona ndio wakombozi wetu wamefunga macho kwenye eneo la uvunjwaji wa katiba na sheria wa wazi unaofanywa na watawala.

Raia tunapaswa kujadili na kuzinduka
 
Kinachostua ni namna ambavyo jamii imekuwa inahadaika kwa urahisi mno.

Hata hawa tunaowaona ndio wakombozi wetu wamefunga macho kwenye eneo la uvunjwaji wa katiba na sheria wa wazi unaofanywa na watawala.

Raia tunapaswa kujadili na kuzinduka

Jiulize kwanza ni kwa nini Elimu ya URAIA inakatazwa kufika maeneo ya kijijini?Je,vijijini wanaelimu ya kutosha ya kuepuka upotoshwaji unaofanywa na viongozi wetu?Je haki za uraia zina tekelezwa vijijini?Watanzania wangapi wanajua haki zao za msingi,kama vile kuhudhuria mikutano ya vyama vya siasa,mikutano ya uchaguzi,kutopigwa na polisi nk.Je,Polisi wenyewe wanajua haki zao na haki za raia wanaowalinda?Ukipata majibu hayo hautakaa ushangae yote yatokeayo Tanzania yetu.
 
Tetty Mwisho wa yote ni NIA ya makusidio mabaya ya watawala kupoka haki za ufahamu za wananchi kwenye nyanja zote.

Watu tunaaminishwa kwamba nchi haiwezi kujiendesha bila misaada ya wanaoitwa Wahisani
 
Last edited by a moderator:
Tetty Mwisho wa yote ni NIA ya makusidio mabaya ya watawala kupoka haki za ufahamu za wananchi kwenye nyanja zote.

Watu tunaaminishwa kwamba nchi haiwezi kujiendesha bila misaada ya wanaoitwa Wahisani

Ni kosa letu watanzania kuchagua viongozi ambao kwa miaka nenda rudi ni wabunge,mawaziri au manaibu waziri na bado tunaenda mbali zaidi kukubali kuchagua mtu sababu tu BABA au MAMA yake alikuwa kiongozi.

Sioni sababu kwa nini tuendelee kuwachagua viongozi ambao kwa miaka zaidi ya 20-40 wao wapo bungeni.Tujiulize kweli hakuna watanzania wenye uwezo?Je tunadhani bila hawa waliopo na familia zao hatuwezi kwenda kule tunakohitaji kwenda.Ni lazima leo kaka Baba Kuku alikuwa Waziri ni lazima Mtoto Kuku awe waziri au mbunge?Je,hatuoni tumejenga taifa lenye fikra mgando sababu viongozi wetu wamefikia mwisho kufikiria,na ndiyo maana wamekuja na dhana bila muwekezaji,mhisani hatuwezi kuendelea.Hivi kweli watanzania tumekuwa wavivu kwa kiasi hicho?

Kinachotusumbua watanzania ni kutokuwa tayari kufanya mabadiliko chanya.Tuanzae sasa kuachana na fikra potofu za kuwa hatuwezi kufanya mabadiliko ya uongozi,tukikubali sisi watanzania kuubadili uongozi leo,basi nina uhakika uwoga wa viongozi wala rushwa utaongezeka na inawezekana rushwa na ufisadi ukapungua.
 
Naam hilo nalo neno.

Hivi ni LAZIMA rais atoke kwenye Baraza la Mawaziri? Kwa nini tumejivika hilo koti bila kujitambua? Vyeo vya kupeana kwa fadhila mwisho wake ni kuipeleka nchi shimoni. Hata siku moja bwanyenye hajui shida ya kabaila
 
Naam hilo nalo neno.

Hivi ni LAZIMA rais atoke kwenye Baraza la Mawaziri? Kwa nini tumejivika hilo koti bila kujitambua? Vyeo vya kupeana kwa fadhila mwisho wake ni kuipeleka nchi shimoni. Hata siku moja bwanyenye hajui shida ya kabaila

Tunaoelewa tumejivika koti la uvyama,udini na mlengo gani mtu upo.Tumekosa uzalendo kile kibaya kilichofanywa na kiongozi sababu tu tunamapenzi naye tunaliona ni jema na tunalipigia debe.Mfano mzuri ni kauli ya Rais wetu ,je kuna uhalali wa kuikubali kauli yake?Kwa nini waliokaribu naye wasimwambie ukweli kuwa Mheshimiwa hapo umepotoka?Je,wanamuogopa?Hivyo inabidi kubadilika sisi tunaoelewa kauli au kitenda kibaya tusikipigie makofi bali tukipigie kelele.Na tukumbuke hata ukitenda mema mengi lakini baya dogo litakuwa kubwa kuliko mema kumi uliyoyafanya.Daima mtu hatazamwi kwa mema bali kwa mabaya,basi kauli na vitendo vyetu sote tuviangalie visije vikaliingiza taifa letu kwenye misguano isiyo na tija.Viongozi ni binadamu wanakosea inabidi tuwasahihishe.

Mimi,wewe na yeye wote ni viongozi katika nyanja tofauti tuanza kujirekebisha ili tuiokoe nchi na taifa letu tuwe wazalendo tuwe na utaifa.Vyama vyaweza,kufa ,mimi na wewe pia twaweza kufa lakini Tanzania itabaki.Tuwatendee haki kizazi chatu kijacho,wasije wakafukua makaburi yetu kuangalia kama vichwa vyetu vilikuwa na ubongo au maji.Wasije wakaona tembo katika picha na sanamu.Waikute misitu na milima yetu.

Tubadilike tuache unazi wa vyama,udini,ukabila au ukanda.Tanzania yetu sote haibagui.
 
....Tubadilike tuache unazi wa vyama,udini,ukabila au ukanda.Tanzania yetu sote haibagui.
Linapokuja suala la mtawala kufanya mambo ya HOVYO, hakuna anayethubutu kumshauri wala kumuonya replication ya matendo yake. Kauli aliyotoa rais ni mwendelezo wa ile ya Pinda na ni mwendelezo wa usiginaji wa Katiba kwa kupoka haki za watu na kufanya watakavyo. Ni sawa na mtoto mdogo achukue bastola ya baba aende kucheza nayo......

Upofu wetu umetokana na mapenzi ya kijinga ya vyama ambapo tunatengeneza ushabiki usio na tija kwa nchi. Mwaka mzima wananchi wanalazimishwa kufanya siasa Januari to Disemba.

Dhamana kwa vigezo vya peremende na kulindana hazitaisha hadi labda tubadilishe mfumo....
 
Hakuna kiongozi au mtawala ambaye hapendi atawale
miaka yote ya uhai wake wewe si unaona kule kwa Mugabe

wengi wanapenda sana vyeo na wanapenda kutawala sana
tena wanatawala kwa udikteta na ukandamizaji
 
Msanii ili viongozi wabadilike kwanza watawaliwa tunatakiwa kubadilika vinginevyo kunyonywa na kunyang'anywa haki za msingi kwa kisingizio cha viongozi kujua zaidi kitakachotokea kuliko sisi wenyewe .Tunapofurahia kupeleka majeshi yetu nchi za wenzetu tujiulize na sisi je tupo salama?

Watanzania kwa sasa tunahitaji kubadilika vinginevyo tusitegemee mabadiliko chanya ya mfumo wetu wa siasa, maendeleo,afya na elimu. Katiba inatuonyesha watanzania tuna haki ya kufuata chama chochote cha siasa tujiulize leo je,haki hiyo serikali yetu na viongozi wetu wanaijua?Watu wangapi wamekwisha kufa toka vyama vya siasa vimeanza?

Tunatakiwa kuwapigia kelele hawa walioshika mpini sasa imetosha tupewe haki zetu zote za msingi,za kusikilizwa,kuamua,kuamini na kufuata kile tunachodhani ni sawa mradi tu hakuna sheria inayovunjwa.
 
....Tunatakiwa kuwapigia kelele hawa walioshika mpini sasa imetosha tupewe haki zetu zote za msingi,za kusikilizwa,kuamua,kuamini na kufuata kile tunachodhani ni sawa mradi tu hakuna sheria inayovunjwa.
Nani aliyewapa uwezo wa kushika huo MPINI?

Naungana na hoja yako. Cha msingi ni kutoa elimu zaidi na kuwashirikisha watu kufanya maamuzi ya busara kwa ajili ya nchi yao. Kuna wahuni wachache ambao wanaamini wana akili kupita watu wote hivyo wanajipa jukumu la kuamua watakavyo...

Tufike mahala neno HAPANA libebe maana hiyo
 
Nani aliyewapa uwezo wa kushika huo MPINI?

Tufike mahala neno HAPANA libebe maana hiyo

Tuliowapa kushika mpini ni sisi watanzania,na tunaotakiwa kusema HAPANA ni sisi watanzania,lakini wengi wetu HAPANA yetu ni NDIYO,hapo ndipo tunapotofautiana.Na kwa uhakika angalia hata baadhi yetu michango yetu kwa mambo ya kitaifa yakoje,je tunayazungumza kwa umakini,uwazi na ukweli.Hatuangalii aliyetoa hoja nzuri yupo chama gani,na kwa sababu chama chake siyo chetu tunaishia kumkejeli na kumtukana?

Mitandao ya kijamii ndiyo ingekuwa ya kwanza kupeleka taarifa ya nini hatukipendi watanzania lakini elimu hiyo inafika?Au tunaishia kutukanana wenyewe kwa wenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…