Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,914
- 3,437
Asubuhi njema rafiki yangu.
Nina imani umeianza siku hii ya leo vyema, ukiwa tayari umeipangilia ili kuweza kutumia muda wako vizuri.
Kama bado hujaipangilia siku hii, basi fanya hivyo kwanza kabla hujaendelea kupoteza muda wako.
Na kuipangilia siku hii huhitaji kufanya makubwa sana, chagua tu mambo matatu muhimu unayotaka kuyakamilisha siku ya leo na anza kuyafanya hayo kabla hujafanya mengine.
Karibu kwenye tafakari yetu ya leo ambapo leo tunakwenda kutafakari kuhusu VICIOUS CYCLE au kwa kiswahili MZUNGUKO WA MATATIZO.
Hii ni dhana tata ambayo imekuwa inawafanya watu kushindwa kubadili maisha yao na kupata mafanikio.
Katika mzunguko huu wa matatizo, tatizo moja linazaa tatizo jingine ambalo tatizo hilo linakurudisha kwenye tatizo la nyuma. Kwa hiyo unajikita unazunguka hapo hapo kwenye matatizo hayo mpaka mwisho wa maisha yako.
Mifano ya VICIOUS CYCLE kwenye maisha yetu..
1. Umasikini na afya mbovu.
Mtu ambaye ni masikini anakuwa na maisha ya chin hivyo anakosa vyakula bora na anaishi kwenye mazingira mabovu. Haya yanapelekea afya yake kudhoofu na kuumwa. Anapoumwa anahitaji kutibiwa, hivyo anakwenda kutumia hata kile kihela kidogo alichokuwa anapata. Hii inamzidishia umasikini na inapelekea afya yake kuwa mbaya zaidi.
2. Madeni na umasikini.
Mtu ambaye ni masikini, kipato chake hakimtoshelezi, na hivyo njia ya haraka ni kukopa. Lakini anapokopa anahitajika kulipa mkopo na riba, hivyo anatoa hela nyingi kuliko alizopokea, hii inazidi kumdidimiza kwenye umasikini, anarudi kukopa tena na mzunguko unaendelea.
3. Kukosa maarifa na maisha magumu.
Mtu ambaye hana maarifa sahihi anakuwa na maisha magumu, hii ni kwa sababu anafanya maamuzi mabovu mara zote. Anapofanya maamuzi haya mabovu anakazana kuyarekebisha bila hata kujipa maarifa, hivyo anakosa maarifa na anarudia tena matatizo yale yale.
Kuna mifano mingi mno ya MIZUNGUKO YA MATATIZO, ni imani yangu kwamba umepata picha halisi na namna gani mizunguko hii imekuwa inaendelea kwenye maisha yako.
Yatafakari maisha yako na itambue mizunguko hii kisha chukua hatua.
Na hatua ya kuchukua ni kuvunja huu mzungukom BREAK THE CYCLE.
Unavunjia wapi? Huo ni uamuzi wako mwenyewe, uzuri huu ni mzunguko hivyo unaweza kuvunjia popote.
Ila ili uweze kuvunja mzunguko huu, ni lazima uwe tayari kuishi maisha ambayo hujawahi kuyaishi hapo awali. Ni kazima uwe tayari kujitesa kwa muda mfupi ili kuyaweka sawa maisha yako ya muda mrefu.
Vunja mzunguko wako wa matatizo leo, na ishi maisha ya uhuru yenye furaha na mafanikio. Yote yanawezekana.
Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
www.makirita.info
#MUHIMU; Kupata tafakari hizi kila siku pamoja na makala za mafanikio kwenye KAZI, BIASHARA NA MAISHA KWA UJUMLA, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga tuma ujumbe kwa njianya wasap wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwenye namba 0717396253 na utapewa maelekezo. Karibu sana.
Nina imani umeianza siku hii ya leo vyema, ukiwa tayari umeipangilia ili kuweza kutumia muda wako vizuri.
Kama bado hujaipangilia siku hii, basi fanya hivyo kwanza kabla hujaendelea kupoteza muda wako.
Na kuipangilia siku hii huhitaji kufanya makubwa sana, chagua tu mambo matatu muhimu unayotaka kuyakamilisha siku ya leo na anza kuyafanya hayo kabla hujafanya mengine.
Karibu kwenye tafakari yetu ya leo ambapo leo tunakwenda kutafakari kuhusu VICIOUS CYCLE au kwa kiswahili MZUNGUKO WA MATATIZO.Hii ni dhana tata ambayo imekuwa inawafanya watu kushindwa kubadili maisha yao na kupata mafanikio.
Katika mzunguko huu wa matatizo, tatizo moja linazaa tatizo jingine ambalo tatizo hilo linakurudisha kwenye tatizo la nyuma. Kwa hiyo unajikita unazunguka hapo hapo kwenye matatizo hayo mpaka mwisho wa maisha yako.
Mifano ya VICIOUS CYCLE kwenye maisha yetu..1. Umasikini na afya mbovu.
Mtu ambaye ni masikini anakuwa na maisha ya chin hivyo anakosa vyakula bora na anaishi kwenye mazingira mabovu. Haya yanapelekea afya yake kudhoofu na kuumwa. Anapoumwa anahitaji kutibiwa, hivyo anakwenda kutumia hata kile kihela kidogo alichokuwa anapata. Hii inamzidishia umasikini na inapelekea afya yake kuwa mbaya zaidi.
2. Madeni na umasikini.
Mtu ambaye ni masikini, kipato chake hakimtoshelezi, na hivyo njia ya haraka ni kukopa. Lakini anapokopa anahitajika kulipa mkopo na riba, hivyo anatoa hela nyingi kuliko alizopokea, hii inazidi kumdidimiza kwenye umasikini, anarudi kukopa tena na mzunguko unaendelea.
3. Kukosa maarifa na maisha magumu.
Mtu ambaye hana maarifa sahihi anakuwa na maisha magumu, hii ni kwa sababu anafanya maamuzi mabovu mara zote. Anapofanya maamuzi haya mabovu anakazana kuyarekebisha bila hata kujipa maarifa, hivyo anakosa maarifa na anarudia tena matatizo yale yale.
Kuna mifano mingi mno ya MIZUNGUKO YA MATATIZO, ni imani yangu kwamba umepata picha halisi na namna gani mizunguko hii imekuwa inaendelea kwenye maisha yako.Yatafakari maisha yako na itambue mizunguko hii kisha chukua hatua.
Na hatua ya kuchukua ni kuvunja huu mzungukom BREAK THE CYCLE.Unavunjia wapi? Huo ni uamuzi wako mwenyewe, uzuri huu ni mzunguko hivyo unaweza kuvunjia popote.
Ila ili uweze kuvunja mzunguko huu, ni lazima uwe tayari kuishi maisha ambayo hujawahi kuyaishi hapo awali. Ni kazima uwe tayari kujitesa kwa muda mfupi ili kuyaweka sawa maisha yako ya muda mrefu.
Vunja mzunguko wako wa matatizo leo, na ishi maisha ya uhuru yenye furaha na mafanikio. Yote yanawezekana.Nakutakia siku njema sana.