Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,407
Habari za asubuhi rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo umepata nafasi ya kuianza. Ni siku ambayo una nafasi ya kwenda kuweka ubora zaidi kwenye chochote unachofanya ili kupata matokeo bora zaidi.
Wakati unafurahia kuanza kwa siku hii mpya ya leo, naomba utafakari kwa kina sana sababu ya kukutoa kitandani leo.
Kwa nini umetoka kitandani leo? Ni kitu gani kimekusukuma uache shuka na kuianza siku yako?
Je umetoka kitandani kwa sababu ya hofu?
Hofu kwamba utachelewa kazini na hivyo kufukuzwa...
Hofu kwamba utawakosa wateja mapema na hivyo kukosa kipato...
Au umetoka kitandani kwa mapenzi?
Mapenzi kwamba leo unakwenda kufanya kazi yako kwa ubora zaidi...
Mapenzi kwamba leo unawahi kuwapatia wateja wako bidhaa na huduma bora sana ambazo hawajawahi kuzipata?
Tafakari kwa kina ni sababu ipi imekutoa kitandani, na leo fanyia kazi sababu hiyo. Kama ni hofu basi fanya kazi ya ziada ili utoke kwenye hofu na kwenda kwenye mapenzi.
Maana kile unachofanya kwa mapenzi mara zote huwa bora kuliko unachofanya kwa hofu.
Kwa vyovyote vile, iwe umeamshwa kwa hofu au mapenzi, nina uhakika, hizi siyo sababu ambazo zimekuamsha leo..
Hukuamka leo ili ufuatilia habari ambazo hata siyo muhimu kwako.
Hukuamka leo ili uende kuharibu siku ya mtu mwingine.
Hukuamka leo ili uzurure kwenye mitandao ya kijamii na kupoteza muda wako.
Hukuamka leo ili ufuatilia habari za udaku na maisha ya wengine.
Hukuamka leo ili uwe sehemu ya wanaoshabikia mambo ambayo hayana faida kwao.
Jua ni kipi kimekuamsha leo na kipe kipaumbele, mengine ni kelele ambazo ukizifuata zitakuchekewesha kufika kulenunakotaka kufika.
Nakutakia siku njema sana.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
#MUHIMU; Kupata tafakari hizi kila siku asubuhi, pamoja na makala nzuri za KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO kila siku, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga tuma ujumbe wenye neno KISIMA CHA MAARIFA kwenye wasap namba 0717396253.
Karibu sana.