Tafakari ya hotuba ya mhe. Rais 31 desemba, 2005

mahangu

Senior Member
Nov 9, 2010
148
59
" I MAY BE WEARING A SMILE BUT IT COULD BE VERY EXCEPTIONAL, I'M FIRM ON ISSUES, NASEMA NINA MSIMAMO KWENYE MASUALA YA MSINGI"

Haya ni maneo ambayo aliyatumia Mhe Rais wetu JK mwaka 2005 Desemba wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maneno hayo yalijenga imani sana kwa Bunge kwa Rais, Wananchi kwa Rais. Tuliowengi tukaanza kufikiria kuwa nyumba za serikali zilizo uzwa kwa usimamizi wa Magufuli zingerudishwa, NBC iliyouzwa bei chee kwa makaburu ingerudishwa, Air Tanzania ingeboreshwa zaidi na kuwa shirika la ndege shindani, walanguzi wangedhibitiwa ( sukari, mafuta, mchele, mahindi n.k), mashirika yaliyouzwa kienyeji na kwa bei chee yangerudishwa, Malala miko ya mzawa Reginald Mengi ya kutendewa ndivyo sivyo katika mchakato wa ubinafsishaji Kilimanjaro Hotel yangeshughulikiwa, wezi wa fedha za EPA wote washughulikiwa, TAKUKURU ingeimarishwa na kuachwa huru, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ingeundwa upwa na kuwa huru kwa mabadiliko ya kifungu cha 98 cha Katiba ya Nchi, Makampuni ya Uchukuzi ya Mikoa ( KAURU, KAUM, KAUDO, IRINGA RETCO, MBEYA RETCO etc) yangefufuniliwa ili kuchochea uchumi, Hospitali za Mikoa na za Rufaa zingeboreshwa kutoa huduma bora na ya kisasa ( Hakuna sababu ya kwenda India) n.k. Haya ndo mambo ambayo kwa tafsiri yangu na imani yangu kuwa ndo ya MSINGI, na ndivyo nilivyo mwelewa Mheshimiwa Rais.

Lakini kama tujuavyo, wahenga walisema " NGOMA IVUMAYO HAIDUMU". Waandishi waliokuwa mstari wa mbele kumtangaza ( e.g akina Kibanda- Mtanzania by then, Badra Massoud-Now Tanesco etc) walijaribu hata kuanza kuhesabu siku za utawala wake, tukaletewa kitu kinaitwa 'SIKU 100 ZA JK IKULU", wakafanya tathmini wakasema mpeni muda zaidi. Hatimaye tumaini jema likaanza kuptea taratibu, tukaanza kusikia makashifa, tukaona rais wetu kimya, kila jambo, kimya. Hapo matumaini ya watanzania tulio wengi yakaanza kupotea taratibu. Ule usemi wa siku ya uzinduzi wa bunge ukapotea jumla kwa mhe. Rais, mambo ya msingi ( kama nilivyorodhesha hapo juu) kwa kiasi kikubwa yakaachwa, watanzania tukabaki na matatizo yetu.

Swali kwa Mhe Rais, je yale mambo ya msingi uliyokuwa ukiyasema kwa ule usemi wako pale Bungeni desemba 31 ni yapi? mimi ni mwananchi wa kawaidi ningependa kujua kabla hujaondoka 2015, ili wanahabari waliokupamba sana 2005 wasije kuchafua sana wakati umepumzika na familia yako baada ya kazi ngumu ya urais.

Samahani wana JF kwa post ndefu lakini nilitaka kuwakumbusheni kutafakari usemi huo wa Rais

Mwenye macho haambiwi Tazama
 
Nakumbuka John Cheyo alisema hiyo ilikuwa the best speech aliyowahi kuisikia, ilitoa matumaini sana kwa Watanzania kwa kweli. Inabidi mheshimiwa aisikilize yeye mwenyewe tena ili atafakari pale alipokosea ajirekebishe ndani ya muda uliobakia.
 
Huwezi kuona kama hujayaandaa macho kuona, huwezi kusikia japo masikio unayo na siyo kiziwi kama hujaandaa masiko kusikia, Mtu hawezi kukubali ukweli kama hajajiandaa kukubali. Upo usemi unaosema "MOYO UNAONA ZAIDI KULIKO MACHO" na natambua kuwa wote wanaobeza kila linalofanywa na Serikali ya JK sivyo ambavyo mioyo yao inavyoona. Mioyo yao lazima itakuwa inaona wapi Rais ameweza, wapi ameshindwa na kwa sababu gani. Chuki binafsi, maneno ya kubeza na mengine mengi ni umbo la nje tu la watanzania wachache ambao hata hivyo macho ya mioyo yao inashindana na umbo hili za nje.
 
Baada ya hotuba hiyo (hopeful iliandaliwa na serikali iliokua inatoka madarakani) akaanza sasa kutuandikia muhtasari wa safari zake " wiki iliyopita nilikua marekani, wenzetu wamefurahishwa sana na mkakati wetu wa kupunguza vifo vya mama na mtoto wamenipa zawadi"

"nikaonana na watanzania waishio marekani nikawaambia waje kuwekeza nyumbani hata kama si mali basi nyumba"
(hotuba yake ya mwezi september hiyo)

WATANZANIA WANATAKA SUKARI MAJI SAFI MAFUTA,BARA BARA NZURI, HUDUMA BORA ZA AFYA we unatoa muhtasari wa anasa zako ughaibuni na kukenua kama umechomekwa midoginga masaburini, this ugly oldman bwana, very mbumbumbu
 
Back
Top Bottom