Tafakari: Urafiki mbaya......kuuvua.

Tafakari: Urafiki mbaya......kuuvua.

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Kituo cha 10.
Yesu anavuliwa nguo.
Eee Yesu tunakuabudu tunakushukuru, kwakuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu.

Askari wanamvua kwa nguvu nguo zake zilizogandamana na madonda, wanayaamsha mara moja mateso yote aliyoteswa tangu mwanzo.

Eeh Yesu uliyevuliwa nguo iliyogandamana na madonda, upate kunifundisha kuuvua kwa nguvu urafiki mbaya au kitu chochote kinachoharibu urafiki na Mungu hata ikinipasa kutoa sadaka kubwa.

Wapendwa wanaMMU tunaujua urafiki mbaya? Kwa sala hiyo ya njia ya msalaba ni ULE UNAOHARIBU MAHUSIANO YAKO NA MUNGU, na mwisho wa siku hauwezi kuwa na mwisho mzuri kwako. Na mara karibu na zote, huwa unaumiza kuuacha maana kuna gains tulizokuwa tunazipata tukuuvua basi tutazipoteza (sadaka kubwa).

Jumapili na kwaresma njema.
 
Urafiki ni matokeo ya ubinadamu kutoweka duniani!
 
Mbona sijaelewa.

Urafiki ni zao la binadamu kuuacha ubinadamu

Binadamu baada ya kuuacha ubinadamu walitengeneza mahusiano yasiyohusisha ngono ili kufarijiana na kusaidiana kwani binadamu hutegemeana

Hapo ndipo kitu kinachoitwa urafiki ulipopatikana!
 
Kwa ubinadamu unamaanisha Utu? Na waliuachaje? Kwa dhambi ya mwanzoni? I mean ya Adamu na Eva?

Waweza toa mifano ya urafiki mbaya ambao unavutia?
 
Kwa ubinadamu unamaanisha Utu? Na waliuachaje? Kwa dhambi ya mwanzoni? I mean ya Adamu na Eva?

Waweza toa mifano ya urafiki mbaya ambao unavutia?

Ndio namaanisha utu

Waliuacha pale walipomkosea Mungu wao

Yaani hivi
Mungu nalipowaumba wote wawili aliwaagiza wapendane,kupenda kulikomaanishwa hapa sio kule kwa kingono bali ni kumkubali mwenzako bila hata kuweka sharti lolote lile ndio maana hata Adam aliupoletewa Eve alimkubali yaani alimpenda bila kujiuliza maswali ya hovyo kama huyu ni mwembamba au ni mnene n.k bali alimkubali kama alivyo

Walipokosea walitengeneza njia ya kujiunganisha na uovu [Shetani] kwa kujichafua hivyo wanatoka kwenye utakatifu na kuingia kwenye hali nyingine kabisa,tangu siku hiyo walikuwa wameuacha utu

Kama ilivyo kawaida Shetani yeye alaiga vile ambavyo Mungu ameviweka na kutengeneza vya kufanana na hivyo.kwakuwa Mungu aliweka Upendo yeye akaleta urafiki ambao nao kama ulivyo upendo una misingi yake

Tofauti na ilivyo upendo ambao wenyewe umeagiza wanadamu kukubaliana bila kuwekeana masharti upendo wenyewe ukawa na kuwekeana masharti.Hii maana yake ni kwamba wewe Kaunga nikisikia unaumwa sitajiuliza chochote nitakuja kukuona na kukupa msaada ule ulioko kwenye uwezo wangu na kuondoka bila kukudai chochote kile,huo ni upendo lakini kwenye urafiki nikisikia mtu anaumwa kama sio rafiki yangu basi sitajisumbua kwenda kwasababu sio rafiki yangu,huo ni urafiki

Kwa haraka haraka unaweza kuona vile ambavyo urafiki unavyotenganisha watu na upendo unavyoweza kuunganisha watu bila kuweka kipingamizi chochote

Nadhani kwa maelezo hayo mafupi unaweza kupata angalau point ya nilichokuwa nazungumza

Pia napenda nikujuze tu kuwa wakati naandika haya umeme umekatika mara 4 na nimerudia ndio maana umeona nimechelewa kukujibu sijui ni kwanini lakini hatimae nimefanikiwa,jina la bwana libarikiwe!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa neno la kiroho hasa kweny hii kwaresma ....
 
Very true, urafiki mbaya una gharama sana kuuvua, sijui kwa nini.

Lakini kuna muda inabidi tu usimamie maamuzi yako, kama upo na urafiki na unakuzuia kuwa karibu na Mungu wako, bora kuondoka, na ili usinaguke tena, basi jarinu kutorudi nyuma asilani.
 
Si unajua shetani anavyoweka sukari vitu vyake. Sasa huyu mchumba sugu nafanyaje, maana kwaresma hii naweza mmvua lkn baada ya kwaresma sintaendeleza kamchezo kweli?
 
He he he, ni kazi sana. Ila fanya maamuzi ya kukamilisha safari, oaneni kama hamna vizuizi na kama mmeridhiana.

Uchumba sugu huwa unatesa sana, ila siku mkikamilisha inaleta faraja sana, ndo hapo mtu unaanza kuwaza kuokoka kabisa.

Si unajua shetani anavyoweka sukari vitu vyake. Sasa huyu mchumba sugu nafanyaje, maana kwaresma hii naweza mmvua lkn baada ya kwaresma sintaendeleza kamchezo kweli?
 
Maneno kama haya ungetuhabarisha kila siku hapa jukwaani siyo kusubiria hadi kwaresma. Bt thanx alot.
 
Back
Top Bottom