Ndugu yangu Mmaroroi, soma hizo bolds, ukiweka kichwani kuwa inawezekana, utaweza hata kwa kuanzia chini, sio lazima mkopo tu save taratibu na uwekeze hatua kwa hatua inawezekana tu. Kwani kina Peacock walikua na ajira, elimu, mikopo mikubwa? na wengineo walioanzia chini.
Jaribu pia kufanya vitu kwa kufuata sheria anzia na biashara ndogo, huku umeajiriwa, mikopo pia inapatikana kwa biashara ndogo mf Grocery, duka, nyumba zenye hati hata za kata wanapokea, mifugo: kuku, ngo'mbe.
Ukiwa na positive attitude utafanikiwa lakini ukikazania kuwa haiwezekani ndo basi tena. Mie nilikimbizia hiyo mikopo wee, nimeacha, sasa hivi nimeanza mifugo yangu itoshe matumizi yangu ya mwezi, then matumizi + fees ya mtoto, then matumizi + fees yangu + ya mtoto = Nisiwe tegemezi tena kwa mshahara ili niwekeze kwenye vitu vingine.
BADILIKA