Tafakari fupi Miaka 61 ya Uhuru

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Tanganyika inaadhimisha miaka 61 ya uhuru tangu kuondoka kwa wakoloni wa Kiingereza nchini mnamo 1961.
Tanganyika imepiga hatua katika Mambo mbalimbali bàada ya Uhuru huo kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Mabadiliko katika huduma za jamii yamekuwa chachu katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja ingawaje bado kuna changamoto.

Kuboreshwa kwa Mazingira ya kibiashara kumeliwezesha taifa kupiga hatua kiuchumi kutokana na mapato yatokanayo na uwekezaji wa viwanda, kilimo na shughuli mbalimbali Barabara zenye urefu wa zaidi ya km 11, 000 zimejengwa kwa kiwango Cha lami nchi nzima.

Ununuzi wa ndege za umma za abiria zaidi ya 10 mpaka Sasa pamoja na ujenzi wa meli 14 zinazotoa huduma katika Maeneo mbalimbali nchini.

Kuboreshwa kwa Mazingira ya utoaji elimu na maendeleo ya elimu ya juu ambapo vyuo vya umma takribani 30 vimejengwa nchi nzima.

Maendeleo haya sio haba yanapaswa kupongezwa na kuhimiza juhudi ili yaweze kusonga mbele zaidi.

Tukizingatia hayo tunapaswa pia kutathmini usahihi wa hatua yuliyopiga, changamoto na Vikwazo ambavyo taifa linavikabiri kufikia miaka 50 ya uhuru.

Je, mifumo ya kiuchumi tuliyonayo inakidhi matakwa ya Taifa, inatusaidia kukua kimaendeleo?
Utoaji wa huduma unaendena na umri wa taifa hili huru lenye utajiri wa kila aina ya rasilimali?.

Je, mifumo yetu ya siasa ni rafiki na inakidhi matakwa ya mfumo wa demokrasia ambao Tanzania inauunga mkono duniani?

Maendeleo ya mtu mmoja mmoja yanaakisi ukweli takwimu zilizopo?.

Tafakari hii iendelee kwa mawanda mapana na kutoa suluhisho kwa wakuu wa Jamhuri hii kuangalia ni namna gani taifa lisonge mbele zaidi tutoke hapa tulipo Daktari mmoja kuhudumia watu 20,000 mpaka watu 3,000 ambao ndio wastani angalau.

Yote kwa yote Heri ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Taifa hili Tukufu.

Peter Mwaihola kitaaluma Ni Mwandishi, Mhariri Wa Habari na Mchambuzi.
 
Back
Top Bottom