Tafadhalini nisaidieni jamani mamaangu (strock) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhalini nisaidieni jamani mamaangu (strock)

Discussion in 'JF Doctor' started by KIBURUDISHO, Nov 15, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  WanaJF wenzangu habari za majukumu tafadhali naombeni kwa wanaofahamu tiba ya ugonjwa huu wa kupooza upande mmoja uliompata mama yangu anateseka.Kwa mara ya kwanza ulimtokea mwezi wa 5 akapewa dawa za kienyeji akapata nafuu.Lakini ilipofika leo asubuhi hiyo hali imejirudia upya yaani anapitisha tu udenda tunaambiwa ugonjwa huu haupaswi mgonjwa akadungwa sindano sasa najiuliza wapi nitakapopata tiba ya kumponya mamaangu naombeni ushauri wenu.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,606
  Trophy Points: 280
  Diagnosing stroke

  Huo ni ugonjwa wa khatari sana na ugonjwa huu hauwezekani na madawa yoyote isipokuwa yale ya kienyeji tu, kwani hospitalini wameshashindwa. Pole sana.

  a.Ama kwa huduma ya kwanza tumia, udil karaha kwa wingi,Habbat soda unga vijiko vitano,Asali vijiko vitano, Hii ni kwa ajili ya kula, Ama kwa ajili ya kupakaa ni mafuta ya zaituni vijiko viwili 1x2 wiki moja.

  b.Tiba kwa ukamilifu kwa idhni ya Allah:
  1.Bakalhad
  2.manimani
  3.Ubani dhukra
  4.mustaki
  5.kungu manga
  6.habbati soda
  7.sufa
  8.kakila
  9.makul az-rak(buma)
  10.basbas jauza
  11.halilinji
  12.balinji
  13.albinji
  14.tangawizi kavu
  15.daarfilfil
  16.hiliki
  17.haltiti
  18.maka udi karah
  19.Vyote mchanganyiko Twanga Uchekeche upate unga wake kisha Uchanganye kwenye Asali Safi mbichi kipimo cha chupa moja na nusu. Awe anakunywa hiyo Dawa kwenye kikombe cha kahawa kila siku kabla ya kula kitu kutwa 1x3 kwa muda wa wiki moja Inshaallah atapona.

  c.Mgonjwa atachuliwa kwa dawa zifuatazo: Menthol,tymol(arak zamda) juice ya kitunguu thaumu nusu kikombe cha kahawa, mafuta ya zaituni kikombe cha kahawa koroga sawa sawa kutwa 1x2 Mumchue kwa hizo Dawa kwa muda wa mwezi mmoja.

  D. Dawa zinapatikana Kariakoo kwenye Maduka ya Dawa za kiarabu karibu na soko kuu la Kariakoo, waulize wapemba watakufahamisha wapi zinapatikana. Tumia kisha unipe mimi maelezo mgonjwa anaendeleaje. Please Give me a FeedBack.
   
 3. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa kuwaona neurologists au neurosurgeons ili wamfanyie examination zinazotakiwa kuangalia kama ni reversible.
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole ndugu yangu sina msaada cjasomea hvyo vitu,Mungu amponye mama na kumpa afya njema,
   
 5. N

  Nehondo JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kamuone daktari mtaalamu wa mambo hayo kuna mama anaitwa prof lutale wa muhimbili akushauri
   
 6. e

  estano New Member

  #6
  Apr 24, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba msaada naomba kufahamu.
  Ndugu yangu ana KOVU KWENYE UBONGO,imesababisha kupata stroke upande wa kulia,tiba yake ni nini,hasa kutibu hili kovu kwenye ubongo na stroke,ana miaka 6 sasa tangu augue.
  Asanteni.
   
 7. REX

  REX JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2013
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  matatizo haya yote mara nyingi yanatokea kwa wenye umri mkubwa, na sababu hasa ni mfumo wetu wa maisha ambao tumekuwa nao, wenzetu wazungu wanahama kwenye huo mfumo lakin kwa bahati mbaya sis ndio kwaza tunaingia,tatizo la kisukari na presha ndizo zinazoo ngoza kwa kusababisha matatizo haya na kwa kiwango kidogo ukimwi japo siyo sana
  kuwa mzito kupindukia ni moja ya sababu za kupata hizo stroke, jaribu kuangalia wenzetu wanavyokabiliana nayo na usisubiri mpaka ufike huko maana ni vitu vichache unaweza kusaidiwa muda ni sasa Natural Health and Beauty
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,606
  Trophy Points: 280
  Mkuu estano Mwambie atumie Dawa zangu hizo hapo nilizoweka juu kwa muda wa siku 21 Mfululizo inshllah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu atamponyesha tumia hizo Dawa kisha uje hapa unipe Feedback.


  Kipigo - Stroke

  Kipigo ni nini?

  Pia huitwa ugonjwa wa kuvamia bongo. Hutokea wakati ambapo mishipa ya damu ubongoni mwa mtu huziba na kupasuka na kufanya baadhi ya seli (Cells) za ubongo kufa. Hizi seli za ubongoni zinapokufa, shughuli ambazo sehemu

  hiyo ya ubongo hudhibiti hupotea. Hizi ni pamoja na uwezo wa kuongea, kusonga, na kukumbuka vitu. Iwapo unazitambua dalili enenda hospitalini haraka iwezekanavyo kwa matibabu. Kupata matibabu haraka kunamaanisha kuwa kuna nafasi bora ya kupona kabisa.


  Ni zipi dalili za kipigo?


  • Kupooza au kufa ganzi kwa uso, mkono ama mguu, hasa kwa upande mmoja tu wa mwili
  • Kuchanganyikiwa kupata shida kuongea au kuelewa mambo
  • Shida ya kuona ukitumia jicho moja au yote
  • Shida ya kutembea. Kizunguzungu au kushindwa kufikiri vizuri na kusawazisha mambo
  • Kuumwa na kichwa pasipo kutambua kiini
  • Kichefuchefu cha ghafla, kuwa na homa na kutapika kwa dakika au hata masaa
  • Kuzirai, kuchanganyikiwa, kifafa ama kuzimia kwa muda


  Unawezaje kuzuia ugonjwa huu?


  • Ni muhimu shinikizo lako la damu likaguliwe mara kwa mara iwapo liko juu kuna uwezekano mkubwa wako kupata ugonjwa wa kipigo.
  • Fanya mazoezi na ule chakula kisicho na mafuta mengi. Pia kiwe na chumvi kidogo
  • Chunguza iwapo mpigo wako wa moyo uko sawa. Utahitaji tiba ya kupunguza uwezekano wako kupata ugonjwa wa kipigo
  • Wacha kuvuta sigara mara moja. Huzidisha mara dufu uwezekano wa kupata ugonjwa huu
  • Iwapo wewe hulewa, punguza kipimo hadi chupa mbili tu kwa siku.
  • Punguza kiwango cha ‘cholesterolÂ’ mwilini na ni muhimu ikaguliwe kila mara
  • Iwapo una ugonjwa wa Sukari, dhibiti na uchunge sana aina ya chakula unachokula.
  • Iwapo una shida na kuzunguka kwa damu mwilini, tibiwa.

  Unatibuje ugonjwa wa kipigo?


  Iwapo una mojawapo wa hizi dalili, hata kama hazisababishi uchungu au zikitokea hupotea haraka, unaweza kudhibiti kuharibika kwa ubongo wako. Iwapo kuna uzibaji au kuvuja kwa damu, daktari atajaribu kuvitibu kwa dawa au upasuaji.

  Watu wengi ambao wamewahi kupata ugonjwa wa kipigo, huwa wanalazimika kujifunza kutembea tena. Mwanzoni,

  wanapoendelea kupata nafuu huwa hawakumbuki vitu ama hata wao hushindwa kusongeza baadhi ya sehemu za miili yao.

  Kupona huchukua muda, ni kibarua, huhitaji msaada na utulivu. Watu wengi huhitaji utunzi maalumu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. K

  Kifyatu JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2013
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,919
  Likes Received: 1,831
  Trophy Points: 280
  Mimi namuunga mkono ndugu yangu Dr. MziziMkavu.

  Zaidi ya hapo niongeze tu kuwa kwa kawaida tufe (lobe) la kushoto la ubongo linahimili upande wa kulia wa mwili, na la kulia linahimili kushoto kwa mwili. Kwa viumbe wengi tufe la kushoto la ubongo pia linahimili maongezi.

  Kama mtu amepooza upande wa kushoto wa mwili hii ina maana tufe lake la kulia (the subconscious home) ndio lililopata pigo. Hawa watu huwa hawana matizo ya kuzungumza ila tu wanaathirika zaidi njozi zao na wanaweza kuendelea na maisha kama kawaida. Zaidi ya tiba zilizotolewa, mamacheza (physical therapy) ya viungo ni muhimu.

  Kama mtu amepooza upande wa kulia wa mwili hii ina maana tufe lake la kushoto (the conscious & speech home) ndio lilopata pigo. Hawa watu huwa na taahira ya mazungumzo (speech). Mamacheza (Speech + physical therapy) ni muhimu.

  Neuro-specialists please saidia.

  Poleni sana mnaouguliwa. Sote tunaelekea huko kwa njia moja au nyingine.
  Hii ni njia ya Marhaba, haina mmoja
  .
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Pamoja na madawa ya kiasili nakushauri umuwahishe hospitali. Baba yangu alipata stroke 2004 na akagundulika ana kisukari hapo hapo. Alipona kabisa stroke na hadi sasa anahudhuria hypertension and diabetes clinic. Kwa control ya diet tu hadi sasa hatumii vidonge vyovyote na ana afya njema. Msikate tamaa atapona tu.
   
Loading...