Jay Milionea
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 1,185
- 154
Maeneo ya Kijitonyama karibu na hotel ya Grand Villa ambayo pia ni maeneo linapojengwa kanisa, kuna nyumba ambayo kwa mbele ina geti nyeusi kubwa na dogo. Hayo mageti yanatumika kutapeli watu wakidhani yanaingia ndani kumbe ukiingia ni uchochoro tu ambao watu wengi wanapita lakini huwezi jua jinsi palivyo.
Sasa hii namba 0674-644233 haijasajiliwa nashangaa tiGO inawachaje watu wanatumia namba bila kusajiliwa? Haina jina na inatapeli sana watu wengi kila kukicha, inauma sana na huyo mtumiaji akishakutapeli anajigamba kwa kukuambia kuwa huo ni uchochoro sio nyumba ya mtu kisha anazima simu, baadae anawasha tena.
Naomba/nashauri vyombo husika vimfatilie huyu mtumiaji watu wanalizwa jamani na huyo tapeli tena ana vijana wake ambao ndo anawatumia kuseti ramani za kutapeli lakini eneo hilo la uchochoro ndilo litumikalo.
Chonde chonde mnaotumia mtandao wa kupatana huyo jamaa ndo adui yenu mkubwa sana maana anakwambia chukua boda boda kabisa uwahi kumbe unaenda kutapeliwa.
Jinsi anavyotapeli:
Huyo jamaa anatumia Kupatana kama sehemu ya kuibia watu, ukiwa na bidhaa yako anajifanya kutaka kuinunua, kisha anakwambia chukua boda fasta kuna kijana utakutana nae muoneshe huo mzigo kisha atakupeleka kwa mke wangu then yeye atakupa hela yote maana mi niko mbali na mke wangu ni mjamzito.
Kwahiyo ukikubali unapelekwa katika hiyo nyumba ambayo upande wa mbili kuna hayo mageti lkn sio mageti ni uchochoro anakwambia nipe huo mzigo niingie ndani nisubiri hapa dk 1 natoka wewe kwavile ni mgeni na unaona kabisa anaingia ndani ya hiyo nyumba kumbe ndo umeliwa mwenzio kule nyuma kuna uchochoro anatokomea huko, we ukiingia ndani kwavile unahc kachelewa hukuti kitu, ukiuliza wenyeji hapo wanakwambia hii njia watu wanatumia kupita.
Ndo hivyo na wengi wameshalizwa sana