Tabora yasajili vitambulisho vya Taifa

Tabora yasajili vitambulisho vya Taifa

Juma Jongo

New Member
Joined
Feb 14, 2018
Posts
4
Reaction score
1
USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WASHIKA KASI TABORA

Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) imeendelea kufanya vizuri zoezi la usajili wa Vitambulisho Vya Taifa Mkoani Tabora ambapo Wilaya zote zinafanya zoezi hilo. Afisa Usajili wa Mkoa wa Tabora Bi Grace Msaky amesema kuwa wananchi wamelipokea vizuri zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu ili kupata vitambulisho vya Taifa. Grace amesisitiza kuwa zoezi hilo ni muhimu hivyo wanachi wanapofikiwa kwenye kata zao wajitokeze wote kwa wingi ili kukamilisha mchakato huo.

Pia Mwakilishi wa kitengo cha Habari NIDA makao Makuu. Bw. Deodatus Mchaki amesisitiza kuwa Zoezi hilo ni BURE hivyo Mwananchi hatakiwi kuchangia garamayoyote.

Ili kusajiliwa ni lazima Mwananchi afike na nakala (copy) ya nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

Wananchi wanweza kuwasiliana na NIDA moja kwa moja na kituo cha huduma kwa mteja kwa namba; 0673333444/0687416666, 0779102010, 0743201020, 0765201020, ama namba isiyo na tozo 0800758888, Tuandikie S.L.P 12324, Barua pepe; nida.tanzania@nida.go.tz

1.jpg

Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni tayari kufanya HAtua ya pili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

5.jpg

Shaban Yasin mkazi wa mtaa wa Nane nane kata ya Ipuli akichukuliwa alama za Vidole (fingerprint) kwenye zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa
 
Niulize kidogo hiv vitambukisho hutoka baada ya mda gani manake hata mm nimejiandikisha toka mwaka Jana mwezi October lkn mpk leo cjaona wito wa kuitwa nikachukue
 
View attachment 710073
Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni tayari kufanya HAtua ya pili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

View attachment 710074
Shaban Yasin mkazi wa mtaa wa Nane nane kata ya Ipuli akichukuliwa alama za Vidole (fingerprint) kwenye zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa
Na mimi nimeipata hii habari ikawa inazingua kuwa uploaded. Asante Mtoa post na hongera Tabora.
 
Niulize kidogo hiv vitambukisho hutoka baada ya mda gani manake hata mm nimejiandikisha toka mwaka Jana mwezi October lkn mpk leo cjaona wito wa kuitwa nikachukue
Hivi vitambulisho vyao vinatoka baada ya wiki tatu na kuendelea. Niliwahi kufika na kuuliza ofisini kwao wakati nafuatilia cha kwangu. kwamba wamesema wiki tatu mbona imechelewa. Wakanielewesha kwamba baada ya kukamilisha ule mchakato huwa wanakua na kazi nyingine nyuma ya pazia za kuhakikisha uraia wa mwombaji. Sasa wale walioweka viambatanisho vingi inakua rahisi zaidi. Lakini pia Unapaswa kwenda kufuatilia inawezekana fomu yako hukusaini ama hukugonga mhuri serikali za mitaa ama kuna tatizo lolote ata herufi zikitofautiana kwenye fomu na attachment uloiweka ni tatizo. Nazani kwa uwingi wa watu wanachelewa kuwapigia cm mkarekebishe. Ila ukienda kufuatilia unarahisisha.
 
Hivi vitambulisho vyao vinatoka baada ya wiki tatu na kuendelea. Niliwahi kufika na kuuliza ofisini kwao wakati nafuatilia cha kwangu. kwamba wamesema wiki tatu mbona imechelewa. Wakanielewesha kwamba baada ya kukamilisha ule mchakato huwa wanakua na kazi nyingine nyuma ya pazia za kuhakikisha uraia wa mwombaji. Sasa wake walioweka viambatanisho vingi inakua rahisi zaidi. Lakini pia Unapaswa kwenda kufuatilia inawezekana fomu yako hukusaini ama hukugonga mhuri serikali za mitaa ama kuna tatizo lolote ata herufi zikitofautiana kwenye fomu na attachment uloiweka ni tatizo. Nazani kwa uwingi wa watu wanachelewa kuwapigia cm mkarekebishe. Ila ukienda kufuatilia unarahisisha.
Nilishauliza kwa ofisa kata wa eneo husika akasema vitambukisho vyote havijaletwa so sijui ni kwanini vinachukua mda mrefu sana
 
Back
Top Bottom