Taboos (Miiko) Wakati Tunakua.

Taboos (Miiko) Wakati Tunakua.

fredito13

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2012
Posts
213
Reaction score
146
Haya ni baadhi ya mambo ambayo wakati tulikua tulikua tunaamini ni mwiko kuyafanya! Yaani ukifanya lazima kitu kibaya kikupate (imani)

1. Mvulana ukila kwenye sufuria utaota manyonyo
2. Ukimruka mwenzio anakua mfupi
3. Ukimchungulia mkubwa, unapofuka macho.
4. Ukila kitu cha mdomoni (chenye mate), unapata majipu!

Watoto wa siku hizi hawazijui hizi. Wadau ongezeni zingine.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
usinyooshe kidole kwenye kaburi,
ukimuona albino temea mate kifuani,
ukiitwa usiku na mtu usiyemuona usiitikie.
 
Usipige mluzi usiku.
Marafuku kutaja neno chumvi usiku.
Ni vibaya sana kukutana katikati ya mito.
Marafuku kushona nguo usiku.
 
Hiyo ya kujitemeamate kifuani aisee natamani kuifanya hadi leo. Naogopa albino hadi najisikia aibu. Natafuta rafiki ili niiface hii phobia
usinyooshe kidole kwenye kaburi,
ukimuona albino temea mate kifuani,
ukiitwa usiku na mtu usiyemuona usiitikie.
 
ukitaka mtu asahau kitu unakunja konya au unaweka kijiti kichwan (kwenye nywele)
 
Ukikata kucha usiku basi itapelekea baba yako kufariki
 
Mi huwa naipenda hii ya wachaga kwamba ni vibaya kukaa na pombe! Ukija na pombe yako unatakiwa umpe kwanza aliyeketi akushikie ukae ndo akupe, na ktk hali ya kawaida wkt anakupa lazima umwambie RIA hapo akishapiga kidogo ndo upokee. Hii ni haswa kwa mbege.

Kwenye bia wazee wa kichaga akikuomba umnunulie bia sharti isiwe moja, anakwambia tembo hauawi na mkuki mmoja. Duh, wazee wajanja sana!
 
Hixi mambo zilikua burudani sana! Yaani zinakuzuia kufanya kitu kwa imani kuwa ukifanya basi jambo baya litakutokea.
Watoto wa siku hizi ukiwaambia, mpaka wajaribu na kujua ukweli ndo watafuata! Vinginevyo, siku si nyingi wanaharibu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
ukitaka mtu asahau kitu unakunja konya au unaweka kijiti kichwan (kwenye nywele)
Mkuu hiyo kwenye Red haikuwahi kunisaidia hata kidogo. Nilikuwa nikifanya soo home Maza akikaribia kurudi kutoka kazini nilikuwa natumia hiyo mbinu ili asahau...duuuh lakini matokeo yake nilikuwa nachezea bakora za kifimbo cheza cha mtoto..lol.
 
Ukienda kununua chumvi dukani usiku hutakiwi kusema chumvi inabidi useme 'dawa ya mboga'.
 
Ukiweka sungusungu kwenye manyonyo na akakung'ata basi yatakuwa makubwa. Sasa asipong'ata atakandamiziwa kichwa hadi akate roho.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom