Riadha jr
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 569
- 334
Salamu wakuu
Moja kwa moja niingie kwenye mada binafsi kuna vijitabia vinavokera mbele ya watu mtu atakapojihusisha nazo au kushiriki.
(1) Kusikiliza muziki ama ni kwenye simu au device yoyote mbele za watu kwa sauti isiyo binafsi, hii hutokea sana kwenye mabasi.
(2) Kuongea kwa sauti kali na yenye vitisho kwenye simu mbele za watu.
(3) Kujadili mada za nyumbani kwako kwa sauti kubwa ndani ya gari za umma.
(4) Kutoa vitisho ama kwa kunasibisha au kwa kutaka kujulikana wewe una cheo gani kwenye jamii au una mamlaka ya kuweza kuwazidi watu.
(5) Wamiliki wa magari ya umma(hii sana ni kwa mabasi ya mikoani) kuweka kanda za dini zao ilhali wateja wao ni wa dini tofauti na madhehebu tofauti.
MwanaJF mwenzangu hebu na wewe zianike tabia ambazo hufanywa na watu mbele ya umma zinazokosesha amani wengi-