Tabia za watu walio /wanaoelekea kufanikiwa

Lawzmaker

Member
Feb 27, 2016
19
14
1. Hawana mazungumzo marefu sana. Hii hutokana na kuwa watu hawa huamini kuwa wakisikiliza ndio watapata maarifa mapya na ujuzi zaidi kuliko kuongea, ni mara chache sana kuwakuta wakifanya maongezi ya kusengenya watu wengine zaidi sana hutumia muda wao kusikiliza watu wengine ikiwemo waalimu na watu wenye mafanikio zaidi yao.

2. Wanaufahamu mwingi nje ya kitu walicho/wanachokisomea. Mara nyingi mtu mwerevu akubali kubakia na fani moja tu, kama anasomea ualimu haridhiki tu kubakia na fani moja ya uwalimu bali hatahakikisha na maswala ya kibiashara pia anayaelewa vilivyo, pia kama vile aijamtosha basi hata udereva atajifunza ilimradi tu asibakie na fani moja. Kama ni mwanamke mwerevu atokubali tu awe mama wa nyumbani bali atatumia fursa ya kujishuhulisha na mambo mengine yenye kumnufaisha yeye au familia yake kwa kujifunza hata kushona nguo au kuanzisha kibustani nyuma ya nyumba ili mradi tu awe anajishughulisha.

3. Wanashiriki vilivyo katika shughuli mbalimbali za kijamii. Watu hawa hawatosheki tu na kufanya kazi zao binafsi, bali siku kama za ‘wikiend’ wanajichanganya na kuhakikisha wanahusika vizuri kuijenga jamii yao inayowazunguka. Watu hawa hawakosekani kwenye misiba ya jirani zao, kwenye majanga yeyote yatakayoiathiri jamii basi utawaona wakijaribu kutoa misaada yao kama raia wa kawaida tu bila shuruti. Kwa ufupi wana utu na roho ya huruma kwa wengine.

4. Wanatumia vizuri mitandao ya kijamii. Watu hawa huamini kuwa mitandao ya kijamii ni fursa kubwa kwao kupata na kutoa elimu kwa wengine, kutangaza bidhaa au fani zao. Pia watachangia katika midahalo mitandaoni lengo kubwa ikiwa ni kufahamishana na kujuzana. Hii yote wanaafanya uku wakijali muda wao wa kazi na watajitahidi wawezavyo mitandao ya kijamii isije ikawapotezea muda wao wa kufanya shughuli zingine za kila siku.

5. Hawana neno aiwezekani. Wengi wa watu hawa wanaamini kuwa kila kitu kinawezekana endapo utaamua kuivalia njuga ipasavyo. Na msemo huo ndio unawapa motisha ya kuzidi kufanikio zaidi kwa kila watachokuwa wakiamua kukifanya maishani mwao.hawaishii tu kuamini kuwa kila kila kitu kinaezekana chini ya jua bali pia hutamani kuwafahamisha na wengine juu ya kuamini ivo na kujipa ujasiri juu ya kila waliamualo kulifanya.

6. Wako makini. Watu hawa wanakuwa makini kwa kila kitu watachokifanya, umakini wao huanzia kwenye fikra kisha huandika kile walichokifikiria katika ‘diary’ zao alafu huakikisha kinakuwa kweli kama ilivokusudiwa hapo wali, pia umakini wao mwingine ni kuchunga wakati, lazima wajiwekee ratiba zao binafsi na husimamia walichokikusudia kama walivopanga. Mmojawapo ya watu waliofanikiwa alishawahi kusema “ni bora zaidi kuwahi sehemu uliokusudia masaa matatu kabla kuliko kuchelewa dakika moja”

7. Ni viongozi na waelekezi kwa wengine. Watu wa kundi hili mara nyingi ni viongozi, simaanishi kiongozi wa kupigiwa kura au kiongozi anaeteuliwa, la! Namaanisha ni mtu wa kutizamwa na wengine kama “rolemodo” wao kwa vile tu anavoishi, au anavofanya katika maisha yake ya kila siku.

8. Hawajionyeshi kwa watu. Watu hawapendi kujipendekeza kwa watu wengine kuwa wanafahamu sana, mfano mzuri juzi kati nilikuwa nimekaa kwenye ghafla moja ya mahafali ya association mojawapo ya hapa chuoni kwetu, kuna mdau mmoja kaja kisha akafungua begi akatoa computer yake (PC) ya “apple” akawa yuko bize kweli kama ijatosha vile akatoa na headphones akazivaa. Yote hayo anayafanya uku mgeni rasmi akizungumza lakini yeye hakujali. Mtu kama uyo mimi namuita “mlimbukeni” anajionyesha tu na aikuwa na haja ya yeye kuja eneo kama lile na kufanya vitu kama ivo mbele ya watu wengine ambao kwa namna moja na nyingine wameacha shughuli zao zingine na kuja kuskiliza hotuba ya mgeni rasmi.

9. Ni vigumu kutangaza CV zao labda pakiitajika. Mara nyingi watu hawa hata kama wamesoma shule/vyuo bora au kubwa au hata nje ya nchi basi hawajitangazi ovyo, labda ikatokea tu zikaonekana kwa bahati mbaya, vilevile wanaweza wakawa wamefanya au wanafanya kazi katika mashirika makubwa ya kimataifa lakini hawapendi kujionesha kuwa wako tofauti na watu wengine.

10. Wanatambuwa uwepo wa mola wao mlezi. Watu hawa hawishilii tu kutafuta matakwa ya kidunia bali huenda mbele zaidi na kujikurubisha kwa muumba wao na wanaamini kuwa kila kitu wakifanyacho ipo siku wataulizwa na aliewaleta duiniani. Mara nyingi mungu akiwaruzuku basi hutowa sehemu kwa watu wengine wanaoitajia na kutegemea malipo kwa Allah (s.w). pia hufanya ibada zote muhimu kama ilivyoelekezwa na mtume Muhammad(s.a.w).

11. Wanapenda kusoma sana. Mara nyingine wanapenda kujituma na kusoma juu ya mambo kadha nje kabisa na anachokisomea, mfano yeye anasoma “law with shariah” lakini sio ajabu ukamkuta na vitabu vya kibiashara na yuko seriaz anasoma kweli. Vilevile wanapenda kusoma magazeti ya kila siku sio kwa ajili aonekana ila ni ili ajue kitu gani kinaendelea kitaifa au kimaataifa au kibiashara.
 
kweli kabsa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom