Tabia za Wapigakura na tabia za WanaCCM

Tabia za Wapigakura na tabia za WanaCCM

Joined
Oct 6, 2020
Posts
27
Reaction score
50
TABIA ZA WAPIGA KURA!

1. Mara nyingi sio wazungumzaji sana, hutulizana na jambo lao ndani ya mioyo yao. Sio wapiga kelele, si wapiga DEBE. Uaumuzi wao hujengwa ktk msingi wa SIRI hadi siku ya uchaguzi.

2. Sio watu wa kujitokeza kwenye Kampeni kwa sababu kwao kampeni sio lolote. Uamuzi wao ni matokeo ya msimamo wao wa awali, mara moja moja wanaweza kushiriki kampeni lkn wasibadilike. Wapiga KURA humchagua Kiongozi wao kabla ya Uchaguzi!

3. Sio watu wenye kujimwambafai. Ni wanyonge, wasikivu na wavumilivu sana. Mpiga KURA wa kweli hana mambo mengi, anachojua yeye ni tarehe ya Uchaguzi, basi. Ukimkuta anadeki barabara huyo sio mwenyewe. Huyo ni mpiga kula!

4. Mpiga KURA wa kweli hafuati UPEPO. Hana matusi wala kashfa, anawaheshimu Wagombea wote halafu anamchagua wa kwake kwa SIRI kubwa. Wapiga KURA huwaambii lolote kwa mtu wanaemuelewa!

5. Mpiga KURA anayo agenda. Humchagua mtu kwa kile alichokiona kwa macho sio maneno ya kuambiwa. Wengi hupiga KURA kuchagua matokeo ya maendeleo yao, wengi huchagua matarajio yao kwa kujifunza. Mpiga KURA sio oyaoya, mpiga KURA ni mtu makini kuliko inavyofikiriwa.

TABIA ZA WANA-CCM.

1. Sio lopolopo, ni watu watulivu kwa kuwaona. Mafundisho ya Chama chao hayawataki kufanya vurumai, kupiga kelele. Ni watu wenye heshima, kwao wakati wa Uchaguzi hakuna mbadala wa Chama chao.

2. Ni wavumilivu, wastahimilivu na wasikivu. Kwao kuvumilia hadi saa KUMI jioni tangu saa MBILI asubuhi ili wapige KURA kwa Chama chao ni rahisi mno. Hakuna Chama cha watu wa namna hii zaidi ya CCM Duniani, kama unabisha leta mfano.

3. Ni waaminifu kwa Chama na Serikali. Wakati wa Uchaguzi huungana kwa ajili ya ushindi wa Chama chao. Ni wapiga KURA wa kweli kwa kweli. Hawana longolongo, sio rahisi kubadilisha misimamo yao ktk KURA.

4. Wengi wao wapo vijijini, ni Wazee na akina mama makundi kwa makundi. Kwa wingi wao hawana majivuno wala matashtiti. Hawana mambo mengi siku ya kupiga KURA, ni kupiga KURA tu na kuondoka.

5. Wana-CCM kura huamuliwa na familia. Siku moja kabla ya Uchaguzi Mzee mwenye nyumba husisitiza juu ya CHAGUO la familia, viapo na nadhiri hutolewa hapo. Wale wa vijijini tunafahamu! Kwa Wana-CCM kura zote za familia huangukia kwa Chama, hii ndio siri ya ushindi kwa CCM.

6. Umoja na Mshikamano wakati wa UCHAGUZI ni sifa ya ziada kwa Wana-CCM. Haijalishi kuna tofauti kiasi gani kati yao, Chama kwanza mengine baadae. Hii sifa haiko kokote pale Tanzania.

Msije sema hatukuwaambia mapema, SIFA za wapiga KURA wa kweli ndizo SIFA za Wana-CCM. Kwa lugha rahisi, wapiga KURA wengi ni Wana-CCM. Kwa dhana hii ushindi wa CCM ni kama KIFO.

Endeleeni kusubiri CCM ishinde halafu muandamane ili siku nyingine tujifunze kuacha mambo ya UTANI katika mustakabari wa NCHI.

#LalaSalama!
#MitanoTenaKwaJPM.
MenukaJr.
 
Umenena mkuu! Ila kwa nini umewapa siri hawa chandimu? Wao hapana kura wana mafuriko tu!
 
Maneno yako yamenigusa moja kwa moja mpaka nikahisi unanizungumzia mimi.
 
Back
Top Bottom