Tabia ya kwenda na michepuko kwenye sherehe/harusi

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,493
Siku moja nipo kwenye sherehe ya Harusi nikakutana na jamaa yangu Kalunde kaja na mdada mmoja matata! Yes, we knew alikuwaga side chick wake! Mkewe Kalunde anatokea Mkoa wa wanawake mabaunsa, wamepanda hewani na wadau wa kutoa dozi!

Basi wakati tunatoka like saa 7 hivi mbele yetu Kalunde alikuwa kakumbatia mrembo wake! Hamad! Pande la mama likatokezea kusikojulikana, asee lile timbwili sio la nchi hii! Mdada plus Kalunde walichezea kichapo! Kalunde alitoka speed za Swala huku nyuma jimama likiendelea kumchakaza mrembo wa watu!

Sijui huko nyumbani Kalunde alisolvuje ile case but nilijifunza kitu!

Mheshimu mkeo hata Kama unafanya uchepukaji! Kumpa mwili wako umiriki Side chick ni kujiripua Kama Boko Haram!

Alamsiki!
 
Rafiki yako msukuma kazingua,hajui kwamba harusini mkewe anaweza kuvutiwa waya na wajumbe
 
Back
Top Bottom