Tabia ya kuiba watoto wa shule imeanza

Tabia ya kuiba watoto wa shule imeanza

everybody

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
337
Reaction score
103
Kuna hii habari imekua ikizunguka kupitia text messages kwenye simu na ningependa kujua ukweli wake humu jamvini na kama kuna watu wamekutwa na tukio hili watoe ushuhuda wao ili na sisi wengine wenye watoto wetu mashuleni tujue tunafanyaja. Kwa sasa naona kama habari hii ni ya uzushi tu. Jamani wenye uhakikia tusaidieni. Habari yenyewe inasomeka hivi

"Jamani kuna mchezo wa kuiba watoto wa shule umeanza, kuanzia majuzi watoto 12 wa boko wameibiwa juzi yake watoto 20 wa ununio na wengine wa idadi isyo eleweka wa kunduchi wameibiwa na wote wanaibiwa mashuleni......jana wawili wamepatikana wakiwa wamefariki!! Na inasemekana wamepelekwa mabwepande na mbweni kuna mashimo wanafukiwa na kunyonywa damu....tupendane, mtaarifu na mwenzio!!!

JAMANI KWA WALE WENYE UELEWA ZAIDI TUSAIDIENI
 
pleas mods fowadi hii sms kwa kova haraka sana,ili aweze kulitolea ufafanuzi mapema,maana watu tusha ingiwa na hofu kabisa
 
kama kweli, mbona inatisha kabla yakuona, mmmmh tuwafiche wapi malaika hawa
 
Mi mwenyewe nimesikia hii habari mtaani kuwa kuna watoto wa shule wameibiwa huko boko ila sijajua kama ni kweli ama la may be wenye ushuhuda!!
 
Kuna hii habari imekua ikizunguka kupitia text messages kwenye simu na ningependa kujua ukweli wake humu jamvini na kama kuna watu wamekutwa na tukio hili watoe ushuhuda wao ili na sisi wengine wenye watoto wetu mashuleni tujue tunafanyaja. Kwa sasa naona kama habari hii ni ya uzushi tu. Jamani wenye uhakikia tusaidieni. Habari yenyewe inasomeka hivi

"Jamani kuna mchezo wa kuiba watoto wa shule umeanza, kuanzia majuzi watoto 12 wa boko wameibiwa juzi yake watoto 20 wa ununio na wengine wa idadi isyo eleweka wa kunduchi wameibiwa na wote wanaibiwa mashuleni......jana wawili wamepatikana wakiwa wamefariki!! Na inasemekana wamepelekwa mabwepande na mbweni kuna mashimo wanafukiwa na kunyonywa damu....tupendane, mtaarifu na mwenzio!!!

JAMANI KWA WALE WENYE UELEWA ZAIDI TUSAIDIENI

Watoto wa shule unamaanisha wanafunzi au?
 
Huo ni uzushi... unalenga kupoteza MASS ili msijue yanayojirii Siasa chakavu!! Watoto wapotee mchana kweupe... kwani tupo Somaliya,CAR,au wapi!! hata huko Syria kwenye vita na majangaa hakuna wakupotea hiviivi kijinga!! Tulinde amani na tushiriki kulindana.
 
hata mimi nimpata hiyo sms..nadhani anamaanisha watoto wa primary na wale wa chekechea...nilipoipata tu nikaifoward kwa mkuu wa shule anaposoma mwanangu...inatisha..
 
mimi sijapata hata hiyo sms ngoja niipate huyohuyo aliyenitumia nitamkamata atoe ushahidi
 
Kumbe ni mchezo...
Mie nilidhani ni hali harisi..

AAcha maskhara labda kwa kuwa huna mtoto anayesoma shule za mbaali hapo mjini hii habari ni ya kweli kabisa na pia sisitizieni watoto wasipewe lift. kwa wale wanaovaa kondom kila siku na hawajazaa ndio maana wanaleta utani kwenye mada muhimu kama hii
 
Kuna hii habari imekua ikizunguka kupitia text messages kwenye simu na ningependa kujua ukweli wake humu jamvini na kama kuna watu wamekutwa na tukio hili watoe ushuhuda wao ili na sisi wengine wenye watoto wetu mashuleni tujue tunafanyaja. Kwa sasa naona kama habari hii ni ya uzushi tu. Jamani wenye uhakikia tusaidieni. Habari yenyewe inasomeka hivi

"Jamani kuna mchezo wa kuiba watoto wa shule umeanza, kuanzia majuzi watoto 12 wa boko wameibiwa juzi yake watoto 20 wa ununio na wengine wa idadi isyo eleweka wa kunduchi wameibiwa na wote wanaibiwa mashuleni......jana wawili wamepatikana wakiwa wamefariki!! Na inasemekana wamepelekwa mabwepande na mbweni kuna mashimo wanafukiwa na kunyonywa damu....tupendane, mtaarifu na mwenzio!!!

JAMANI KWA WALE WENYE UELEWA ZAIDI TUSAIDIENI

...soma zaidi:

"Watoto watekwa , walawitiwa na kuteswa kinyama ndani ya handaki lilipo katika msitu wa Mabwepande"

Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.
Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.
Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.
Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.
"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.
"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.
Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.
"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.
"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel
Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.
"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.
"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.
"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.
"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.
"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.
Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.
Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.

-Gazeti la Majira.
11/25/2013
 
Back
Top Bottom