Tabia ya kuegemea magari ya watu

[emoji23] [emoji23]
 
Aisee.....

Mie ningewapa za uso tu

Kwani wakiniona najisikia mchana unageuka usiku???
 
Utaambiwa unaringa

Tatizo kizazi cha siku hizi hakijalelewa kiheshimu mali ya mtu

Nakumbuka enzi zetu uchezee cha mtu utakula fimbo (tena waya) hamu mtu unakuwa huna.....

Unakuta wanamwambia mleta mada gari ya mkopo (sasa si bora amekopesheka?????)
 
Tehe tehe tehe litakuwa gari jipya tu
 
hiyo gari ni aina gani mkuu mpaka unachukia mud akiliegemea!!all ajabu ni vits ndo unasumbua nayo watu!!!kwani ilibadilika rangi baada ya kuliegemea?
 
Ahaha hongera kwa kununua gari mheshimiwa.
 
Kuna watoto nilikuta wamefanya gari langu ubao wa shule.....wamekwangua 1+1=2, 2+2=4......
Bora hao ni watoto. Kwangu sina mtoto mdogo na kazini wote ni watu wazima lakini wamelikwangua kwangua gari hadi huruma. Wakiegemea wanaongea sijui mikononi huwa wameshika nini wanakwaruza weee rangi yenyewe nyeusi huruma tupu. Sio tabia nzuri kusema ukweli.
 
Hawa watoa povu hawajui madhira tunayopata wao wanadhan gari ni kama ndoo ya kuchotea maji
Hawajawahi kumiliki hata baiskeli hawajielewi. Ni uharibifu wa kijinga kuegemea egemea magari ya watu na kuharibu rangi.
 
Gari inayoegemewa taa obviously ni hizi baby walkers kama ni SUV za maana mtu hawezi hata kuisogelea so fight uingie kwenye ulimwengu wa magari.
 
Hawa madogo wa cku hiz akimaliza chuo tu akapata kazi cha kwanza ni gari ananunua hata kabla hajaizoea kazi..mwishowe ni kudata kama hivi
 
Haaaa haaaa nimecheka
 

Tusio na magari tunakomaje? Nawaomba tuwavumilie wenye magari na vichambo na manyanyaso. Usishangae ukiwekewa tambara chini usichafue kapeti la gari, au kufungiwa mlango (ukifunga wewe utaharibu!!!). Usifungue vioo na Ac hawashi. achilia mbali yale maangalizo unayopewa utasikia... huko nyuma kuna laptop ... Gari hii sasa hivi Yadi ni Shilingi Milioni..... ukiagiza nje ni Shiling.... Mafuta ya kuweka shilingi elfu ishirini ishirini yanaharibu pampu... hata kama hujauliza. ole wako usimsifie utaisoma ya JPM.

Mada ya mwenye gari ni mada kuuu usianzishe mada na hata kuchangia kuwa mwangalifu hasa kama mwenye gari yuko na wife/mchepuko utasikia ile saiti ... viza inasumbua sana... exchange rate leo ilikuwa balaa. hivi zile milion tisa alilipa?
NDO SWAGA ZAO.

Kudadeki nimeanza kuweka akiba ya kununulia namimi gari kila mwezi naweka Sh 65,000/- ni mwezi wa tisa sasa. Hivi gari bei gani?

WENYE MAGARI BIG RESPECT KWENU LAKINI MUNGU ANAWAONA !!!!!!
 
pande zetu za disuri mwenye gari akuulizi,.ye anachukua uamuzi wake tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…