Tabia Nane za watu wapole

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
526
Reaction score
903
Tabia nane za watu wa pole.
1. Wanafikiri sana kabla ya kutenda, sio wakurupukaji
2. Ni rahisi kuwaamini
3. Wako tayari kutoa msaada.
4. Ni wazuri kuwa nao kama marafiki
5. Ni wasikilizaji wazuri
6. Wanazielewa hisia za wengine
7. Wanaweza kudumisha mahusiano yao na wengine na ni rahisi kukaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu
8. Ni wagunduzi.
 
HAKUNA WATU WABAYA NA KUWAOGOPA KATIKA DUNIA HII KAMA WATU WAPOLE AISEEE.

HAWA WATU SIKU AKIJA KUKUBADILIKIA NDIO UTAMJUA NI MTU WA AINA GANI YAANI HAWA NI WATU WASHENZI SANA AISEEEE.

MIMI NILIKUWA NINA RAFIKI YANGU MPOLE SANA LAKINI MWISHO WA SIKU ALIKUJA KUNITAPELI HELA YANGU NA AKANIBADILIKIA KAMA SIO YEYE VILEEEE
 
Kweli, ila umesahau moja. Akiishiwa uvumilivu ni mbaya kuliko simba na si wepesi kusamehe.
 
Hapa najiona mimi kabisa
 
Swadakta.
Nimeipenda mno.
 
Huyo sio mpole, alikuwa anakusoma
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu Mpole, Mtaratibu na Mnyenyekevu.

Mtu anaweza kuwa mpole lakini si mtaratibu

Mtu anaweza kuwa mpole lakini hana unyenyekevu.

Mtu mpole ni yule asiye mkali na si Mgomvi.

Ila pia watu wengi wapole wana hekima, Uvumilivu na busara.

Kwa upande wa pili...watu wapole huwa wakireact kwa hasira ni wabaya sanaaa kuliko wale wanaojulikana kuwa ni Wakali.

Pia watu wapole wengi wao ndio wanaowafaidi sana wanawake na pia ndio wanaoongoza kuwa na watoto wa nje ya ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…