Tabia hizi katika Supermarkets zinaboa

Tabia hizi katika Supermarkets zinaboa

Chenji hata kumi nadai ila kama ustarabu hata milioni haina thamani
 
Guys, mleta uzi anapaswa kupewa pongezi. Alichoongea wengi tumeishia kuumia tukashindwa kupaza sauti. Ukweli nchi inapoteza hela nyingi kwa tabia ya aidha kusamehe chenji ama kutopewa kama huyu 98.

Imagine Tanzania ina watu milion 20 wachapakazi na kila mmoja akasamehe ama kutopewa hiyo 100, then zidisha mara 12, then zidisha kwa watu milion 20 tu. See how much tunapoteza , big up 98.
 
Ni vizuri kutumia debit card katika maeneo kama supermarket, kama hauna card basi jitahidi uwe na coins, au ongeza bidhaa nyingine itakayomalizia hiyo mia yako, si busara kwa muhudumu aende kutafuta chenji ilhali kuna watu wengine wanahitaji huduma yake.
 
Mimi nilikwenda Uchumi ya Quality plaza baada ya kufanya manunuzi ya kama 64000, wakaniambia hawana chenji yangu ambayo ilikuwa mia tatu hivi, dada akanishauri nichukuwe chewing gum, nikawaambia sina ratiba hiyo wanipe chenji yangu nisepe.

Wakaanza kuulizana kaunta zote wanadai hawana mara lete mia mbili tukupe mia tano nikawaambia sina, wife akaanza kuwaonea huruma, nikamwambia mpaka nione mwisho wake ukoje, ilichukuwa kama 20min, kumbuka pia hizo pipi unazonunua hazipitii kwenye EFD, kwa hiyo ni wizi fulani hivi.
 
Watu Mia wakiacha Mia 2 daah,100*200....elfu ishirini yupo mbali mno,akifanya mwezi mmoja,fungu la kutosha,mimi hata 50 nadai...
 
sio supermakert tu hiyo tabia ya kutorudsha chenji ipo pale kigongo ferry.hasa wanapoana watu wengi wapo ktk mstari na ferry inakaribia kuondka.ukitoa 500 unaambiwa 100 hawana inabidi uache.kwasababu watu ni wengi nawe unaharaka.ni afadhali serikali iongeze iwe 500.kulkoni wajanja wachache kufaidika na jasho letu
 
Hao hamna tofauti na kubambikwa bill ya beer 2 wakati unakunywa kiroba. Utatamani umtoe mtu utumbo
 
tatizo kubwa liko kwenye bank kuu yetu ambayo haitoi sarafu za kutosha kwenye mzunguko, mimi ni mfanyabiashara ya secreatrial ambayo inahusisha photocopy bei 100 kwa karatasi nimeshazunguka benki zote ikiwemo nmb kuomba sarafu huwa wanajibu hawaletewi sarafu siku hizi hivyo inabidii kununua sarafu kwa bei ya 8000 kwa 10000 hasara ambayo hukutarajia.
 
Mie wakiniletea hizo huwa nawasimamia hadi wanipe, cha kushangaza wanakuwa nazo ila wanadanganya.

Huwa nasema muombe mwenzio etc, siku moja hadi walimwita maneja alete kifuko toka ofisini tena ile ya maeneo ya drive-in wakanipa. Najua wakiniona ni wanajua no kumess nami tena.
 
Ujanja ujanja wa makonda huo...wameiga!

Hahahaha,aisee hii kali.
Ila wengi tunaolalamika ndio hao hao tumeowazoesha.

Wale madada wana tabasam kali,na mtu akienda Supermarket anaenda kinyangema kweli,sasa ukiambiwa hakuna mia unajichekelesha,tehetehetehete,haina shida dada.
Usishangae hata mleta uzi leo tena kaenda kaacha pesa.

Maana ndio Heshma ya Supermarket,tusioweza jamani tununue mitaani,kuna mini supermarket kibaooo,hata change ya hamsini unapewa na vitu ni vilevile.
We umesimama unadai Mia,wakati pembeni kuna mdada yeye kaacha mia nne kabisaa.

Mie nitaendelea kuziacha hizi mia mia saana,maana nimetaka mwenyewe kwenda Supemarket,yaani niambiwe mia sina halafu eti nikomae Counter?aisee acheni zenu wakuu,huko Bar zinaachwa ngapi.
We Supermarket ma Coins ya nini,we huoni baadhi ya bei unaambiwa 99,999,hahaha hujajua tu?

Hembu Zipeni Supermarket heshma,acheni mambo ya vimia mia vyenu,hamuwezi nunue vitu uswahili vipo telee tena bei chee
 
Jana tu Uchumi wamenidhulumu mia tatu yangu, dawa yao ninayo, ni kuanza kuchukuwa zile chocolate karibu na cashier halafu unawaambia wewe pesa iliyopelea utawaletea kesho.

Kuna wengine wana fixed budget. Kuwaambia wachukue chocolate haikuwa kwenye budget yao.
 
yalinikuta haya pale game mliman city. Nilipatwa na mshangao sana mana sikutegemea kukutana na upuuzi kama huo. Sitakubali kuibiwa tena kwa mtindo huu.
 
Mimi ni mteja wa Nakumat hilo tatizo sijawahi kukutana nalo
 
mi nina wallet yangu kizipu cha katikati naweka vi-coins tuuuu, siachi hela, hata 50
 
Hahahah uswahilini hatuendi na mia mia zetu tutadai....

Hahahaha,aisee hii kali.
Ila wengi tunaolalamika ndio hao hao tumeowazoesha.

Wale madada wana tabasam kali,na mtu akienda Supermarket anaenda kinyangema kweli,sasa ukiambiwa hakuna mia unajichekelesha,tehetehetehete,haina shida dada.
Usishangae hata mleta uzi leo tena kaenda kaacha pesa.

Maana ndio Heshma ya Supermarket,tusioweza jamani tununue mitaani,kuna mini supermarket kibaooo,hata change ya hamsini unapewa na vitu ni vilevile.
We umesimama unadai Mia,wakati pembeni kuna mdada yeye kaacha mia nne kabisaa.

Mie nitaendelea kuziacha hizi mia mia saana,maana nimetaka mwenyewe kwenda Supemarket,yaani niambiwe mia sina halafu eti nikomae Counter?aisee acheni zenu wakuu,huko Bar zinaachwa ngapi.
We Supermarket ma Coins ya nini,we huoni baadhi ya bei unaambiwa 99,999,hahaha hujajua tu?

Hembu Zipeni Supermarket heshma,acheni mambo ya vimia mia vyenu,hamuwezi nunue vitu uswahili vipo telee tena bei chee
 
Kama utapenda mrudishie bidhaa ulizonunua na akupe hela yako na uondoke uona kama atakubali na huku kashatoa resiti huwa wanafanya makusudi kwa kuwajua wabongo hawana utaratibu we unaona sh.100 au200 sio hela shauri yenu na hizo supermarikiti zenu
 
Back
Top Bottom