Tabia haibadiliki...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia haibadiliki...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Aug 24, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ukitegemea mchumba wako atabadilika tabia ukishamuoa, jua unajitafutia kujiudhi roho tu. Tabia hazibadilishiki. Kama mwanamke/mwanaume alikuwa mzinzi ataendelea hivyo hivyo hata mkioana.

  Kama mwanamke.mwanaume alikuwa mdokozi, mchoyo, mchafu, mwongo...nk atayaficha makucha yake kwa kipindi fulani kutimiza malengo yake, kisha maisha yataendelea kama kawaida.

  Wazee wetu ndoa zao zilidumu kwakuwa kwenye kutafuta mchumba, walihusishwa wanafamilia na marafiki wa karibu kwenye kutoa ushauri na maamuzi yupi anafaa, au hafai.

  Ndoa za kisasa, waamuzi wa mwanzo na wa mwisho ni wanandoa wenyewe. No wonder ndoa hazidumu.

  Unakubali au unakataa somo hili?

  Jadili.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Waswahili walisema "aisifiaye mvua imemnyea", vipi wewe yamekukuta haya au umefanza kusikia tu?

  Kwangu mimi swali muhimu zaidi ya ama mtu anaweza au hawezi kubadilika, ni lile linalouliza kwa nini utake kumbadilisha mtu? Isn't this selfish and condescending?

  Kwa mfano, mimi sipendi sigareti, na nikijua bibie anavuta sigareti basi ndiyo kwisha habari, hata kumsogelea naona kinyaa. Sasa kwa nini ujue mtu anavuta sigareti, umuingie kwa minajili ya kumuachisha raha yake ya sigareti ili tu awe na wewe? Huu si ukoloni mambopendo huu?
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...:D:D:D definately mazee,

  yameshanikumba sana, huruma tu huniponza

  Unajua, kuna mtu anaweza tenda kosa ambalo 'mwenza' unajiuliza na kuhoji ilikuaje akateleza. Kuna sababu nyingi unazoweza kupewa, mojawapo ikiwa sababu ya upweke, au sikutarajia tutakuja kuoana, au 'vishawishi' vilinizidia... halafu ataapa kwa viapo vyote atavyoweza jiapiza kwamba wala hatarudia tena 'ujinga na upuuzi' ule asije i cost marriage yake.

  Baada ya muda fulani, anarudia tena.

  ..duuuh, kumbe ni starehe yao watu hawa (?), haya bana... No wonder watu wa namna hii ni wasanii kikweli kweli, kwa kujiliza na kutafuta sympathy kabla hujawapa 'red card'.
   
 4. Violet

  Violet Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  True tabia hazibadiliki
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  My point is not so much kwamba tabia hazibadiliki -it is a gamble really, inategemea mambo mengi, lakini kuna mara zinaweza kubadilika-

  My point ni kwamba, kwa nini utake kumbadilisha mtu?

  Hili si gari, kusema kwamba nitalinunua jeupe lakini kwa sababu sipendi rangi nyeupe nitalipaka rangi ya buluu.Au nyumba kwamba nitainunua ya milango minne lakini nitatengeneza mwingine wa tano.

  Kwa nini utake kumbadilisha mtu? huu si ubinafsi uliokubuhu? Mtu anapenda kunywa wewe unataka aache kunywa, Kwa nini uchukue gamble hii? Kwa nini usitafute ambaye hanywi tangu mwanzo?
   
 6. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole mkuu wazee wetu hutwambia hivi ukikutana na mwanamke Bar basi utachana nae bar ukikutana nae magengeni utachana nae magengeni ukikutana mabarabarani mtachana mabarabarabi na ndio manana siku zote ni vyema mtu kuwa na subira na kutafuta wale wenye afuweni ,kuliko kukimbilia hao viruka njia hasara yake ni kubwa ,mkuu kwani hujawahi kukmbana na wasichana lakhai akiwa dukani na kukwambia amepungukiwa alikuwa anataka kununuwa kitu ,na ukimuliza ni kiasi gani amepungukiwa anakwambia laki mbili sasa hapo inakuwa amepungukiwa au hana kabisa ?yamesha nikuta hayo nilipomwambia sina akanambia eti nataka pepo lakini naogopa kufa nikamwambia yake sio pepo ni one way tiketi.
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Bluray, hujawahi sikia wazazi wanatamka, "heri umeoa/umeolewa, umekua sasa", au "umeshakuwa mama/baba sasa, utulie"

  Hiyo haina maana Mke/Mume atambadilisha tabia mwenzake, la hasha. Majukumu mapya (Responsibilities) ndio tegemeo la wazazi hao kubadilishwa tabia. Vivyo hivyo kwenye maisha ya mume na mke, Katu sithubutu kumbadilisha mamsapu tabia, ni jukumu lake yeye mwenyewe kubadilika na kuishi maisha ya ndoa (mke wa mtu).

  Tabia ya (mfano) Uongo, uchafu, uzinzi, nk ndani ya maisha ya ndoa yanafaida gani? Lazima kubadilika.
   
 8. L

  Launoni Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .ukitegemea mchumba wako atabadilika tabia ukishamuoa, jua unajitafutia kujiudhi roho tu. Tabia hazibadilishiki. Kama mwanamke/mwanaume alikuwa mzinzi ataendelea hivyo hivyo hata mkioana.

  Kama mwanamke.mwanaume alikuwa mdokozi, mchoyo, mchafu, mwongo...nk atayaficha makucha yake kwa kipindi fulani kutimiza malengo yake, kisha maisha yataendelea kama kawaida.

  Wazee wetu ndoa zao zilidumu kwakuwa kwenye kutafuta mchumba, walihusishwa wanafamilia na marafiki wa karibu kwenye kutoa ushauri na maamuzi yupi anafaa, au hafai.

  Ndoa za kisasa, waamuzi wa mwanzo na wa mwisho ni wanandoa wenyewe. No wonder ndoa hazidumu.

  Unakubali au unakataa somo hili?

  Jadili.
   
 9. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  nakubali ndoa hazidumu kwa hilo.
  JE NINI KIFANYIKE KUREKEBISHA KASORO HII?
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mimi nadhani familia zihusishwe tu kwenye kutafuta mchumba
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ama kweli wewe ni mvivu wa kufikiri; Yaani umenikopi kule; https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/37029-tabia-haibadiliki.html na kupaste hapa as if umeanzisha thread hii? basi hukuweza hata kubadilisha maneno mawili matatu?

  ...au umetumwa wewe?!
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wazee wetu ndoa zilidumu kwa sababu ya nyakati zao walizoishi.wanawake walikuwa wanatii kila wanachoambiwa ,sio sasa wanawake wengi wameenda shule na wanataka uhuru wa kujaribu mishedede ya size tofauti,na zamani kulikuwa hakuna simu za mkononi au kazi za ofisini kwa wanawake au internet au dvd za porno za kujifunza vitu vipya na kutamani kujaribu. E.t.c kuna mambo mengi yaliyochangia ndoa zamani zidumu ikiwemo kuwakandamiza wanawake........so usisifie mababu zetu tu,hujui full story...
   
Loading...