Taasisi za Usalama wa Taifa zina nguvu kiasi gani?

Haya madude hamna lolote.ni vile tu kwa kuwa hawako wazi.wangekuwa wapo kila sehemu tusingeshuhudia matukio kama vile richmondi,kuletewa treni chakavu itakayotumika sgr,wahuni wasingekuwa wanatamba na kusema hadharani wanalamba asali.vilevile kama wapo kila mahali kusingekuwa na uchaguzi usiokuwa huru na haki.
Kwahiyo unataka kusemaje bwana mkubwa?
 
Kuna vijistori nilivipata mahali, nikaambiwa kwamba hawa jamaa si wa mchezo.

Na hapa nazungumzia kwa ujumla wake, ikiwemo CIA, MOSSAD, TISS na nyinginezo.

Tunaambiwa haya ni madude ya kutisha sana. Ni madubwasha yasiyoonekane yenye maguvu ya ajabu na ya kimiujiza.

Ni madude yenye operesheni za kijasusi kitaifa na kimataifa.

Vile vile yapo kila mahali kama hewa.

Hata ukiwa mgahawani unakula kuku na mchepuko hutakiwi kukohoa kohoa hovyo unaweza ukajikuta mikononi mwao hawa.

Unashtukia tu mtu anachomoa pisto kutoka kibindoni anaitia kwenye paji lako la uso, "unanijua mimi ni nani"?

Halafu lijamaa linairudisha pisto mahali pake na kupangusa pua kama stelingi wa Bongo Muvi kisha linatokomea.

Licha ya maguvu yao ya kimiujiza, tunaambiwa pia yanamfahamu kila mtu nje ndani. Hata ujifiche vipi.

Hii imekaaje?
Intelligence agencies ni vyombo muhimu sana kwa usalama wa nchi ndani na nje.

Zina kazi nyingi sana kuhakikisha nchi haiingiliwi na machafuko na kulindana kuendeleza ustawi wa nchi.

Shida hapa bongo..hicho chombo kinachezewa sana kinajazwa vijana wa kijani..wasio na weredi.

Badala ya kulinda usalaam wa nchi sasa wamegeuka kulinda viongozi wa kijani.

Hii nchi ilipaswa kuwa mbali sana kiuchumi na kimaendeleo ila ndio hivyo tena vyombo vingi vya kulinda na kutetea maslahi ya nchi vimeweka mifukoni mwa wanasiasa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapa kwetu shida ni CCM kujifungamanisha na ttssii Saa ngapi utamwajibisha mtoto wa kada, swahiba! Wanajirambia tu asali kwa kipimo chao.
 
Ngoja nikamuuliza jasusi mbobevu Yericko Nyerere.. Hivi yuko wapi siku hizi haonekani mitandaoni? Amehama kule Mbutu Kigamboni nini?
 
Mossad ni habari nyingine, ukisoma habari zao na operations walizofanikiwa ndio utaelewa binadamu wote ni sawa ni msemo tuu usiweke akilini
 
Intelligence agencies ni vyombo muhimu sana kwa usalama wa nchi ndani na nje.

Zina kazi nyingi sana kuhakikisha nchi haiingiliwi na machafuko na kulindana kuendeleza ustawi wa nchi.

Shida hapa bongo..hicho chombo kinachezewa sana kinajazwa vijana wa kijani..wasio na weredi.

Badala ya kulinda usalaam wa nchi sasa wamegeuka kulinda viongozi wa kijani.

Hii nchi ilipaswa kuwa mbali sana kiuchumi na kimaendeleo ila ndio hivyo tena vyombo vingi vya kulinda na kutetea maslahi ya nchi vimeweka mifukoni mwa wanasiasa.

#MaendeleoHayanaChama
Baba kantuma ndo imeharibu hii nchi
 
Back
Top Bottom