comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Viongozi wa dini wana mamlaka ya juu sana wala hakuna mwenye ubavu wala uwezo wa kuwanyamazisha hata kuwakemea wakihubiri amani, kukemea uonevu na ukatili wowote kwani wao ni wawakilishi wa mungu duniani kupitia mahubiri ya neno la mungu ili dunia iwe ya kistaarabu, amani, utulivu na mahali salama pa kuishi, vilevile ni vioo na alama ya matumaini na amani duniani hasa kwa kukemea,kuhubiri, kuelimisha na kuleta utulivu pale penye sintofahamu au munkari, hivyo basi Maaskofu na Masheikh ingilieni kati matamko kadhaa yanayoashiria kuingilia uhuru wa kutoa na kupata habari, mathalani maaskofu nchini kongo waliwahi kukemea baadhi ya matamko yenye utata na hali ikatulia, baba mtakatifu papa Francis vilevile aliwahi kukemea matamko kadhaa ya kidunia yenye viashiria vibaya hasa vitendo vya uvunjifu wa amani na masuala ndoa, aidha maaskofu nchini Rwanda waliwahi kuhusika na matamko kadhaa ili kuleta amani. Lakini kumekua na ukimya mno hapa kwetu hasa baada ya kuibuka kwa kashfa dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam kuhusu taarifa za kughushi cheti cha kidato cha nne, aidha kumekua viashiria vya kutaka kuingilia uhuru wa kupata na kutoa habari kwa vyombo vya habari pale Mkuu wa Mkoa Daresalaam kuvamia kituo cha habari cha Clouds, maaskofu na mashiekh msikae kimya kabisa hebu toeni tamko la kuweka uwiano wa habari na matamko