Taasisi yataka Lowassa apitishwe kugombea urais

Taasisi yataka Lowassa apitishwe kugombea urais

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeombwa kutumia busara wakati uteuzi wa jina la mgombea urais kwa kupitia chama hicho kuangalia mtu anayependwa na wananchi bila kukiathiri kwa kuteua mtu asiyekubalika.

Wamempendekeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), kuwa ndiye wanayemuona anaefaa kutokana na kukubalika.

Wito huo ulitolewa na taasisi ya Ilawa Improvement ya mkoani Njombe kupitia Mwenyekiti wake, Nathaniel Mgani, ambaye alisema vikao vya CCM vitakapompendekeza mtu atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete iangalie mtu anayekubalika kwa watu ili kutopoteza mvuto wa chama kwa wananchi katika uchuguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

“Kwa niaba ya taasisi yetu tunapendekeza wanapoangalia mtu wa kumuweka kugombea urais wahakikishe wanaweka mtu anayekubalika kwa watu ili kuepuka anguko kubwa, sisi kama Ilawa tunampendekeza Edward Lowassa kuwa mgombe wa urais,” alisema Mgani.

Aidha, alisema wakati Lowassa akiwa waziri mkuu hapakutokea mauaji ya ovyo ya raia wala vurugu katika maeneo nchini.
Mgani alisema Lowassa alipokuwa waziri mkuu hata Rais Jakaya Kikwete hakupata shida kwa kuwa alikuwa na kiongozi aliyekuwa anaisimamia serikali yake na kuwa ilikuwa imetulia.

Aliongeza kuwa wanamuona Lowassa ni kiongozi bora kutokana na alivyosimamia maendeleo katika jimbo lake la Monduli ambalo lina barabara nzuri, huduma za afya na huduma zingine za kijamii zenye uhakika tofauti na maeneo mengine ya nchi.

Aliiomba Kamati Kuu ya CCM kumpitisha Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM kushindana na vyama vya upinzani kutokana na jina lake kuwa masikioni mwa watu wengi na kwa kufanya hivyo chama hicho kitapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
anatafutwa mwenye afadhari kweny group la wachafu. Kama lowasa ndo atafuata basi waliobaki wakoje?
 
Hiyo taasisi ya Ilawa ni kitega uchumi cha CCM au ina interest gani nao? au ina mahusiani gani na CCM?

Haiingii akilini, anyway watu wana tactic nyingi kipindi kama hiki kuelekea uchaguzi
 
Ni kweli kabisa wachague mwenye influence vingnevyo chama kitapotea na wengne hatutak kurudisha kadi..
 
Watanzania tuwe na upeo mkubwa wa kuzungumza hadharani hebu tusubiri wakati ukifika tushawishiwe na watakaojitokeza kugombea huo URAHISI,kwa sasa mnataka apitishishwe Mhe Lowasa, wagombea wengine ambao hawafai ni kina nani?
 
Lowasa anapendwa au anajipendekeza? Ccm hata hivyo msihangaike. Simamisheni yeyote tu msikose ruzuku lakini uongozi wa nchi hatuwapi ng'o!.
 
Back
Top Bottom