Taasisi yamwaga mamilioni kwa `mahausigeli’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taasisi yamwaga mamilioni kwa `mahausigeli’

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TAASISI isiyo ya kiserika inayojishughulisha na kuhudumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na masuala ya jamii, Agape Aids Control Programme (AACP), imetoa sh milioni 16 kwa Kata ya Lubaga, mjini hapa ajili ya kuzuia udhalilishaji, ukatili na unyanyasaji wa watoto wanaofanya kazi za ndani.

  Akitambulisha mradi huo mbele ya Afisa Kazi wa mkoa wa Shinyanga, Charles Byebalilo jana, mratibu wa shirika hilo John Myola alisema, shirika lake limeamua kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wafanyakazi wa ndani kwa kuwa mtoto ni hazina ya serikali, hivyo kwa kumsaidia ataweza kujiajiri kwa kujiingizia kipato chake na serikali kwa ujumla.

  Alisema wameamua kuanza na kata ya Lubaga kwa kuwa inaongoza kwa utoro wa wanafunzi na ni kata inayoongoza kwa kutoa wafanyakazi wengi wa ndani.

  Myola aliongeza kusema kuwa, mradi huo utawasaidia watoto ambao wanafanya kazi za ndani kujiajiri kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakikutana na adha nyingi ikiwa ni pamoja na kudhulumiwa mishahara, kupigwa na kubakwa na baadhi ya akina baba na vijana wa kwenye
  nyumba wanazofanya kazi.

  “Mtoto anayefanya kazi za nyumbani leo, kesho atakuwa mkubwa zaidi na kama hana elimu ya kutosha atafanyaje? Maana itamlazimu kuacha kazi za ndani, ndio maana tumeona tulete mradi huu ili tumpatie ufundi ambao tunaamini utamsaidia kwa kiasi kikubwa kumudu maisha yake hapo baadaye.

  “Katika mradi huu, mtoto atafundishwa ushonaji, kupamba kumbi za harusi kutengeneza batiki na ujasiliamali,” alifafanua mratibu huyo.

  Kwa upande wake, Afisa Kazi wa Mkoa wa Shinyanga, alilishukuru shirika hilo kwa kutambulisha mradi huo na kusema kuwa utaisaidia serikali na Idara ya kazi katika kutokomeza ajira mbaya kwa watoto mkoani Shinyanga.
   
 2. P

  Penguine JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Mwanzo na mwelekeo mzuri. Hata hivyo hao "housegirls" wasitumiwe kama mtaji.
   
Loading...