Taasisi ya kuzuia ukatili kwa wanyama Tanzania

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,420
7,079
Hivi sisi watanzania tumerogwa? Wazee/Vikongwe, Albino wanauliwa tunabaki kucheka cheka, kina mama wanakeketwa, watoto wanabakwa.

Hakuna taasisi maalumu ya kuwashughulikia maswahibu yao, leo hii eti taasisi ya kuzuia ukatili kwa wanyama.
 
Last edited by a moderator:
Taasisi hizi ni katika kutafuta pesa za wafadhili nafikiri ni WAingereza ndo wanaomwaga mi-PAUNDI kufadhili kuzuia ukatili dhidi ya wanyama. U know....
 
Jamii yoyote hupimwa kiwango cha ustaarabu wake kwa kutathmini namna inavyowajali wanyama wake. Kama kulivyo na juhudi za kupambana na manyanyaso dhidi ya makundi ya hao watu katika jamii, kunatakiwa pia juhudi katika kuwalinda wanyama pia kwani nao wanaishi na hawastahili manyanyaso.
 
Mbona walishindwa kuwazuia TWIGA wasipandishwe kwenye Ndege?
Ni sheria ipi inayomkataza twiga kupanda ndege mkuu? Hebu Tufafanulie kidogo. Nachojua ni kwamba kuna sheria zinazoongoza uuzwaji wa nyara za serikali na maliasili kwenda nje, zikikiukwa ndipo upandishwaji wa mnyama katika ndege unapokuwa uvunjifu wa sheria.
Lakini pamoja na maelezo yote hapo juu, hilo halihusiani moja kwa moja na haki za wanyama.
 
Last edited:
Hivi sisi watanzania tumerogwa? Wazee/Vikongwe, Albino wanauliwa tunabaki kucheka cheka, kina mama wanakeketwa, watoto wanabakwa.

Hakuna taasisi maalumu ya kuwashughulikia maswahibu yao leo hii eti taasis ya kuzuia ukatili kwa wanyama.


Umenikumbusha kuna mwaka fulani nilitokea kutembelea Kenya sasa Serikali yao ilitangaza baa la njaa na ni kweli kuna watu walikuwa wanakufa njaa huko Kaskazini mwa nchi yao halafu baadaye nikaona kwenye TV helikopta zinabeba nyati na wanyama wengine kuwapelekea Simba kwenye mapori ya Masai mara kwa kuwa walikosa mawindo!

Hiyo siku sitokuja kuisahau maishani mwangu, hapo ndio nikasema sisi Waafrika inabidi tusimamishe kila kitu na kuanza moja, upya kabisa!
 
Hivi mnajua jinsi KITIMOTO a.k.a OSTAZ PRIDE kinavouwawa kwa NYUNDO tena kichwani. Daah binadamu wakatili sana asee
 
Hivi mnajua jinsi KITIMOTO a.k.a OSTAZ PRIDE kinavouwawa kwa NYUNDO tena kichwani. Daah binadamu wakatili sana asee
Teh teh teh.
Sasa unataka Nguruwe auliwe vipi wakati hana Shingo? Huyu mnyama bila nyundo ya kilo 20 hafi.
Ndio maana Dini ZOTE ZIKAMFANYA HARAMU. lkn Watu wabishi tu.
 
Kuna correlation ya kumjali mnyama na kumjali mwanadam mwenzako....endapo mtoto mdogo anapiga sna wanyama (mkatili) mchunguze utakuta anapiga sana wenzake pia.....
Na hata kuzoea damu ya mauji unaanzia kwa wanyama then unagraduate to human beings.....
Kwa hiyo msipinge pinge kila kitu na hii ni ishara ya uvivu wa kujua mambo na kuishia kukrush kila kitu.
Ukijali haki za wanyama..ukawajali.....trust me mawazo ya kutorture wanadam wenzio itakuwa history,,,.,kasome research za watu walizofanya kuthibitisha hili nilisemalo
 
Back
Top Bottom