Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima: Jipu lililomshinda Ndalichako

choga mkuu

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
283
110
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ni miongoni mwa vyuo vikongwe hapa nchini ambavyo vilianzishwa kwa ajili ya kusaidia jamii kuondoka katika Lindi la ujinga na pia kuwaongezea uzoefu watumishi Wa umma uzoefu ili waweze kufanya kazi kwa ufasaha.

Chuo hiki kilitarajiwa kuendelea kufundisha watu walioko kazini kama ilivyo mtaala unaotumika na chuo hicho, lakini kimekiuka adhima ya kudahili watumishi wa umma na kuanza kuchukua wanafunzi wanaomaliza form six.

Huku katika orientation wanafunzi hawa yaani pre-service wanaaminishwa kuwa Chuo hiki kinafundisha Ualimu kumbe sio kweli maana hakuna course ambazo zinashadadia ualimu kama vile Teaching Methodology na Education Foundation.

Pia chuo hakifundishi namna ya kuandaa Scheme of work &Lesson plan. Wakati wa field practice wanafunzi huchanganywa kila mwaka maana uongozi sometimes huamuru wanafunzi wakafanyie mazoezi ofisini kama vile kwenye Halmashauri na pengine Shuleni.

Sasa chuo kilitoa option kwa wanafunzi kwenye masomo ya kufundishia juu ya kuyasoma,hivyo kuna wanafunzi ambao hawachukui masomo ya kufundishia lakini wanalazimishwa kwenda field shuleni.

Course inayotolewa Bachelor Degree in Adult and Continuing Education haina Code of Service wala Scheme of Service. Wanafunzi kutoka Form six yaan pre-service wanapomaliza masomo yao huwa hawaajiriwi pamoja na kwamba ni course ya ualimu.

Wanafunzi mwezi Wa pili waliandamana mpaka kwa Waziri Wa Elimu lakini jambo hili alionekana kulikwepwa na kukomea kusema "NYIE NI WATU WAZIMA MNAWEZA MKATOKA MKAOMBA VYUO VINGINE".

Jibu kama hili halikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa kama huyu maana vijana wamepoteza muda na pesa .Anapowaambia wakaombe vyuo vingine hela watatoa wapi na ile waliyopoteza pale Taasisi waseme wamepoteza?

Tujiulize kidogo
1)Waziri Wa Elimu anaogopa kuchukua hatua kali juu ya chuo hiki kwa kuwa ni Chuo cha serikali?

2) Mbona wanafunzi kutoka vyuo vya private huwa wanasaidiwa hata kuhama endapo matatizo yanapotokea hasa yanayosababishwa na Chuo?

3) Serikali ipo kuvibana vyuo vya private tu vinapokiuka taratibu za udahili mfano St. Joseph?

4) Wanafunzi kusaidiwa mpaka inapotokea wamegoma na kusababisha madhara makubwa?

Waziri nakuomba utafakari upya ili kuwasaidia vijana hawa ambao taifa linawategemea.
 
Chuo hiki ni moja ya chuo kisichojali utu wa mwanafunzi fikiria tumefungua chuo tangu Tarehe 29 kwa mujibu wa prospectus but tumesaini hela ya chakula na maraz ya Hslb Tarehe 12 but mpaka sasa
 
Haijaingia kwenye Account sijui wanategemea tuishije?
Chuo hiki kila ni tatizo , library tatizo, matokeo tatizo maana huwa wanapanga mpaka GPA ya 5.5 wakati GPA mwisho n 5. Walimu wao wengi wanaofundisha Degree elimu za n bachelor tu . sasa unakuwaje MTU mwenye degree moja anafundisha degree? Boom hucheleweshwa makusudi ili kukumesha wanafunzi, . Chuo hiki n hatari kwa wananchi
 
suala LA course hupaswi kumlaumu WAZIRI, kwani mlichagua wenywe na still mlikuwa na uwezo wa kuhama chuo baada ya kuchaguliwa.
 
Chuo chenu nasikia kilianza kutoa degree bila ruhusa , course zinazotolewa hapo "BACHELOR DEGREE IN ADULT AND CONTINUING EDUCATION haina CODE of service na scheme of service. CHETI nasikia huwa hakina namba kama vyeti vinavyotolewa na vyuo vingine? Mnakazi vijana maana wizara ya Elimu inapambana sana na vyuo vya private ila vyuo vyake haivikagui wala kuvifungia kama walivyofanya St Joseph . Komaeni kiaina
 
Back
Top Bottom